Home Habari za michezo HALI YA KRAMO IKO HIVI SIO WIKI MBILI TENA

HALI YA KRAMO IKO HIVI SIO WIKI MBILI TENA

Habari za Simba

TAARIFA njema kwa mashabiki wa Simba kuwa winga wao Muivory Coast, Aubin Kramo amepata nafuu ya majeraha yake na atarejea uwanjani baada ya wiki moja na sio mbili tena.

Kiungo huyo hivi karibuni alipata majeraha ya goti, kabla ya kurejea nyumbani Ivory Coast kwa ajili ya kwenda kujitibia baada ya kupewa ruhusa kwa mabosi wake.

Nyota huyo alikuwa akisumbuliwa na majeraha hayo mara kwa mara tangu ajiunge na timu hiyo, katika usajili mkubwa wa msimu huu akitokea Asec Mimosas ya nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu winga huyo anatarajiwa kurejea Jijini Dar es Salaam wiki hii sambamba na kuanza mazoezi ya pamoja na timu.

Aliongeza kwa kurejea kwa winga huyo kutaimarisha kikosi hicho, na kumfanya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbrazili Roberto Oliviera ‘Robertinho’ awe na wigo mpana wa kuchagua wachezaji wa kuwapanga.

“Habari njema kwa mashabiki wa Simba, kuwa winga wetu Kramo anaendelea kujiuguza majeraha yake nyumbani kwao Ivory Coast, mchezaji huyo aliumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Ngome FC.
“Na atarejea Dar es Salaam wiki ijayo, tayari kwa kuanza kuipambania timu inayojiandaa na mchezo wake wa marudiano dhidi ya Power Dynamos ya nchini Zambia.

“Hivyo mashabiki wajiandae kupata burudani kutoka kwa Kramo ambaye, wengi wao wanatamani kukuona akionyesha ubora wake katika michezo ijayo,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo Robetinho alisema kuwa: “Kramo anaendelea vizuri kwa mujibu wa madaktari wetu waliofanya mawasiliano naye akiwa Ivory Coast, ninaamini atarejea akiwa imara.”

SOMA NA HII  GAMONDI HUYU ANATAKA KUFUATA NYAYO ZA MANARA!?