Habari za Simba leo
Habari za michezo

SIMBA HALI SI SHWARI LIGI KUU…… NAMUNGO WAFANYA UKATILI WA KULAZIMISHANA

Staff Desk November 10, 2023 12:22 am

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Namungo mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Novemba 9 Uwanja wa Uhuru.

Katika mchezo huo ambao Simba walikuwa chini ya Benchi jipya la ufundi baada ya kuondoka kwa Mbrazil Robertinho siku chache zilizopita.

Namungo ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la uongozi kipindi cha kwanza kupitia kwa Reliant Lusajo dakika ya 28.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika Namungo walikuwa mbele kwa uongozi wa bao 1-0.

Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko kadhaa na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Jean Baleke akimaliza pasi safi kutoka kwa Moses Phiri.

Kwa matokeo hayo Simba wanafikisha alama 19 baada ya michezo 8 huku Namungo wakifikisha alama 8 baada ya michezo tisa katika nafasi ya 10.

AZIZ KI AMUIBUA KOCHA MFARANSA KWA HILI LA CHAMA NI WAZI MAMBO SIO MAMBO MSIMU HUU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply