Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club imewataarifu wanachama wake kuwa Mkutano Mkuu wa Mwaka utafanyika Jumapili Desemba 21, 2023 katika Ukumbi wa Julius Nyerere International Centre (JNICC).
Kwa mujibu wa barua waliyoichapisha kwenye ukurasa wao wa Instagram, ajenda za Mkutano huo zimeainishwa katika ibara ya 22 ya Katiba ya Simba Sports Club, 218. Taarifa hiyo imeeleza pia kufuatia maelekezo ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), moja wapo wa ajenda itakayojadiliwa ni mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya Simba SC hivyo Bodi imeunda Kamati Maalum ya kuratibu mchakato wa Marekebisho ya Katiba.
Bodi imewaalika wanachama wenye mapendekezo ya marekebisho ya katiba wayawasilishe katika ofisi za Sekretarieti au kupitia barua pepe ya simbasc.co.tz kabla ya Desemba 30, 2023.