Home Habari za michezo MBINU HII INAYOTUMIWA NA TFF DHIDI YA SIMBA NA YANGA…YATUMIWA KWA PSG...

MBINU HII INAYOTUMIWA NA TFF DHIDI YA SIMBA NA YANGA…YATUMIWA KWA PSG YA UFARANSA..

Habari za Simba leo

Kumekuwa na utaratibu au kawaida ya mechi mbalimbali kusogezwa mbele au kubadilishwa kwa ratiba ili kuzipa muda wa maandalizi zaidi Simba na Yanga kwenye mechi za CAF

Msimu huu pia kabla ya Yanga kucheza na Mamelodi sundowns pamoja na Simba kucheza na Al Ahly robo fainali za klabu bingwa hilo pia lilitokea kwa kusogezwa mbele au kubadilishwa ratiba ili kuwapa maandakizi mazuri kwa Simba na Yanga kuziendea mechi hizo muhimu

Kama ulijua ni Afrika pekee hayo huwa yanatokea basi huenda taarifa ya PSG kutocheza mechi mbili za ligi ili kujianda na mechi za nusu fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Borussia Dortmund zitakupa kitu kuhusu umuhimu wa mashirikisho kuzipa muda wa maandalizi timu zao kwenye michezo muhimu

Mechi ya April 27 dhidi ya Le Havre na ile May 4 dhidi ya Nice zote zimeahirishwa ili kupisha michezo miwili ya nusu fainali dhidi ya Dortmund zitakazochezwa April 30 pamoja ule mchezo wa marejeano utakaopigwa May 7

SOMA NA HII  KAMA WEWE NI MPENZI WA SOKA KWELI...SASA SIKIA HII KUTOKA INFINIX....UKIPATA NOTE 12 VIP LEO HII UNAJIBEBEA NA DStv...