Home Habari za Yanga Leo FIFA YAIFUNGULIA YANGA KUSAJILI…WAANZA NA JITU LA MAGOLI

FIFA YAIFUNGULIA YANGA KUSAJILI…WAANZA NA JITU LA MAGOLI

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeiondolea Yanga SC adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kukamilisha malipo ya aliyekuwa mchezaji wao Mzambia Lazarus Kambole.

Kitendo cha Yanga SC kundolewa katika adhabu hiyo wamepata uraisi wa kumsajili kiungo mshambuliaji Clatous Chama wanayehusishwa nae kumsajili katika dirisha hili.

Kambole alifungua kesi hiyo FIFA dhidi ya Yanga SC kwa kushindwa kumlipa ujira wake na alishinda kesi hiyo.

Baada ya Kambole kushinda Yanga SC ilitakiwa kumlipa nyota huyo ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa, lakini haikutekeleza amuzi huo na kusababisha ifungiwe kusajili.

Baada ya kukamilisha malipo hayo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungulia Yanga SC kufanya uhamisho wa ndani wa wachezaji.

Awali klabu hiyo ilifungiwa kusajili baada ya kuwepo kwa madai ya mchezaji huyo wa Zambia ambaye alivunjiwa mkataba wake mwaka jana.

Sasa Yanga wanaweza kuanza kusajili na kutambulisha wachezaji wao wapya, ambapo hadi sasa iwa taarifa zilizopo tayari nafasi muhimu zinazohitaji watu zimeshakamilika.

Nafasi ya beki wa kushoto, beki wa kati, kiungo wa ulinzi wa kusaidiana na Aucho, winga, na nafasi ya ushambuliaji ambapo kwa habarinza uhakika ni kwamba tayari Yanga imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Al Nasr ya Libya na Raia wa Ghana Jonathan Sowah.

Huku pia wakikamilisha usajili wa kiungo wa ulinzi Adolf Mtasingwa kutoka klabu ya Azam FC, kwa mkataba wa miaka miwili.

SOMA NA HII  MABINGWA WOTE WA MASHINDANO YA CAF NI KUJICHOTEA MABILIONI YA PESA...SIMBA WAKIKAZA TU WAMO...