Home Habari za Simba Leo FREDY KOUABLAN TOP SCORER…AFIKISHA MABAO 22 SIMBA SC

FREDY KOUABLAN TOP SCORER…AFIKISHA MABAO 22 SIMBA SC

Freddy Kouablan

Anaitwa Freddy Michael Kouablan mshambuliaji wa Simba SC rasmi alimeibuka mfungaji bora wa Ligi kuu ya Zambia, baada ya kufunga jumla ya mabao 14 alipokuwa akikipiga kwenye Ligi hiyo, klabu ya Green Eagles kabla ya kujiunga na Mnyama dirisha dogo.

Raia huyo wa Ivory Coast (25) amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo, baada ya kuwashindani wenzake kadhaa akiwemo mshambuliaji wa Zesco United Enock Sakala mwenye mabao 12, Adrew Phiri anayekipiga Muza FC (11), Ricky Banda na Saddam Banda wote wanakipiga klabu ya Red Arrows wamefungana kwa idadi sawa ya mabao (10). Ambapo pazi la msimu wa 2023/24 limetatika rasmi hii leo.

Freddy Kouablan huenda ndiyo ukawa usajili mzuri zaidi wa Simba kwenye dirisha dogo, kwani tangu atue klabuni hapo amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 8 akifanikiwa kumfikia mshambuliaji mwenzake, ambaye aliondoka klabuni hapo Jean Othos Baleke.

Mashabiki wengi wa Soka la Bongo haswa wapenzi wa Simba SC, wamegawanyika kimtazamo kuhusu mchezaji huyu, wapo wanaosema ni mchezaji mzuri apewe muda atakuwa ni hatari sana, lakini kuna wengine wanasema Freddy Kouablan hafai kuvaa jezi ya Simba kiwango chake ni kidogo.

MPIRA UHESHIMIWE.

Mchezo wa mpira wa miguu ni mchezo wa wazi na kila mtu anauona, lakini wengi hutofautiana uelewa na namna ya kuutazama mchezo huo.

Mchezaji yeyote hupimwa kwa namba na mchango wake kwenye timu, anapokuwa na mpira na pale anapokuwa hana mpira.

Kwa upande Freddy Kouablan ni moja ya washambuliaji wazuri sana anapokuwa na mpira na pale anapokuwa hana mpira huwa anakuwa na mikimbio hatari ambayo huwakimbia mabeki wa timu pinzani ili kutengeneza “space” nafasi kwa viungo wake kuona mashimo na kuweka pasi zenye hatari kwenye eneo la tatu la mpinzani.

Tangu atue Simba amecheza nusu msimu tu na kufunga magoli 8 na hapo akiwa kwenye Ligi mpya hivyo mazingira ni mapya, akimkaribia Saidoo Ntibazonkiza ambaye ndiye Top Scorer wa klabu hiyo akiwa na mabao 10 kwenye Ligi.

Kwa kuhitimisha iko hivi Mashabiki wa Simba wanatikiwa kuwa na subra na mchezaji huyu, mpeni muda wa kuizoea Ligi, azoeane na wenzake, atafutiwe viungo wazuri nafikiri mtamuimba sana, Freddy Kouablan tuupe nafasi muda, utaamua zaidi juu ya uwezo wa huyu mchezaji.

SOMA NA HII  WIKIENDI YA KUTAJIRIKA NA MKEKA WA MERIDIANBET NI HII HAPA...ODDS ZOTE KALI NI HIZI...