Home Habari za Simba Leo SIMBA YAMUWEKEA NGUMU CHAMA… MO HAMUHITAJI TENA

SIMBA YAMUWEKEA NGUMU CHAMA… MO HAMUHITAJI TENA

Habari za Simba leo, Clatous Chama

Mwamba wa Lusaka ni jina lilitamba sana na linaendelea kutamba hadi sasa, mitaa ya Kariakoo Msimbazi na Jangwani, kwa habari za kuaminika kabisa ni kwamba, Clatous Chama bado hajasaini mkataba mpya na Klabu ya Simba SC, licha ya  kuhusishwa zaidi na kujiunga Klabu ya Yanga.

Yanga SC wamempa ofa nzuri zaidi Chama, kuliko ambayo amepwa na waajiri wake wa sasa, Simba SC lakini bado hajasaini pia kwa upande wa Yanga.

Inaelezwa kwamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC, Salim Abdallah “Try Again” anataka kumpa mkataba mpya mchezaji huyo na kumfanya aendelee kukipiga katika klabu ya Simba, lakini kuna changamoto kwa mwekezaji MO Dewji ambaye sasa anaona kuwa inatosha kwa Clatous Chama kuendelea kuhudumu katika Klabu ya Simba.

Hadi ambapo taarifa hii inaandikwa, Klabu ya Simba inaonekana kujitenga na suala la Clatous Chama na wako tayari kumruhusu aondoke kwa sababu idadi kubwa ya wajumbe wa Bodi ya Simba wanaona kuwa inatosha kwa Chama na Simba kuhudumu mitaa ya Msimbazi.

Mohammed Dewji mapema hii leo, inaelezwa kwamba amerudi kwa kasi kubwa kwenye kuiapoti timu hiyo kiuchumi ili irejeshe makali yake,  na ametoa ahadi ya kuedelea kufanya kazi kwa   kushirikiana na Uongozi wa sasa.

Klabu ya Simba kupitia Mwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi wamepanga kusajili wachezaji wazuri lakini vijana ambao watakuwa Simba kwa muda mrefu. Na kwa kuthibbitisha hilo  wameanza na sajili ya Elie Mpanzu kutoka AS Vita huku wakimnyapia kwa ukaribu zaidi beki wa kati wa Yanga Bakari Mwamnyeto.

Msimu uliomalizika wa 2023/24 haukuwa mzuri kwa Simba SC, kwani hawajachukua kombe lolote kubwa la ndani isipokuwa Ngao  ya Hisani, na Kombe la Muungano,  huku kimataifa wakiishia hatua ya  robo fainali.

SOMA NA HII  RAGE AMPIGA TWISHENI KOCHA SIMBA...AWAFUNDISHA WACHEZAJI NA MAKOCHA... ISHU NZIMA IKO HIVI