Home Habari za Simba Leo IDD PAZI AMSHAGAA BOCCO KUACHA MPIRA…MANULA AMPA MBINU

IDD PAZI AMSHAGAA BOCCO KUACHA MPIRA…MANULA AMPA MBINU

Habari za Simba SC

ALIYEWAHI kuwa Kipa wa Taifa Stars, Simba na Majimaji ya Songea Idd Pazi ameshangazwa na uamuzi wa John Bocco kustaafu soka mapema, huku akimshauri kitu Aish Manula baada ya kukaa nje kipindi kirefu.

Idd Pazi, alisema Bocco alikuwa na nafasi ya kuendelea kucheza kama asingesikiliza kelele za mashabiki.

Pia amewapa ushauri wachezaji wengine kukaza kama wanavyofanya kila Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Shomary Kapombe na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.

Kipa huyo wa kwanza kufunga bao katika Dabi ya Kariakoo mwaka 1984 katika sare ya 1-1 dhidi ya Yanga, alisema wapo baadhi ya wachezaji wazawa wanaoonekana umri umewatupa mkono, ila anaamini wakienda nchi jirani watang’ara kama wageni wenye umri mkubwa wanvyong’ara nchini.

Pazi alisema taarifa za Bocco kustaafishwa zimemshtua kwani anaamini angeendelea kucheza soka katika nchini za Kusini mwa Afrika ikiwamo Afrika Kusini, anaamini angeng’ara na angeendelea kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars.

“Ukiachana na Bocco, kuna Kelvin Yondani, Erasto Nyoni,Shomari Kapombe, Salum Abubakar ‘Sure Boy na wengine wengi ambao bado wana uwezo mkubwa uwanjani ni wakati wao wa kwenda kushang’ara nchi za watu kwa vipaji walivyonavyo,” alisema kipa huyo wa zamani wa El Merrikh ya Sudan na kuongeza;

“Nimewashuhudia wachezaji wengi wa kigeni katika ligi yetu, wenye umri mkubwa na wanafanya vizuri, mfano Fabrice Ngoma, Yannick Bangala, Khalid Aucho, Meddie Kagere, Ley Matampi, hao nchini kwao walionekana wamemaliza, sasa kwa nini sisi wa kwetu, wanashindwa kujaribu.”

Akimzungumza hatma ya Aishi Manula kuendelea kuitwa Tanzania One, kuona ipo mikono mwa Simba na Azam FC, vinginevyo afanye maamuzi magumu ya kwenda nje.

“Kama Simba ikimuacha Manula na Azam haitamchukua, akienda timu ambazo zinashika nafasi kuanzia ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu, kuna ubora kwake utapungua, hapo Aishi atapaswa afanye maamuzi magumu ya kwenda nje,” alisema Idd Pazi, Father.

SOMA NA HII  MUDA WOWOTE BALEKE KUTAMBULISHWA YANGA...STORI IKO HIVI