Home Habari za Simba Leo MAZITO YAIBUKA, COASTAL UNION WARUDISHA PESA ZA SIMBA…USAJILI WA LAMECK  LAWI

MAZITO YAIBUKA, COASTAL UNION WARUDISHA PESA ZA SIMBA…USAJILI WA LAMECK  LAWI

LAMECK

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Coastal Union zinaeleza kuwa fedha ambayo klabu ya Simba iliingiza kwenye akaunti ya Coastal Union kwaajili ya biashara ya mchezaji wao, Lameck Lawi zimerudishwa kwenye akaunti ya Simba baada ya biashara hiyo kwenda tofauti na makubaliano ya pande zote mbili.

Moja kati ya watu wa ndani wa klabu ameeleza kuwa Simba walipewa tarehe ambayo walipaswa kufanya malipo ya shilingi milioni 205 ambazo ni fedha za usajili wa mchezaji huyo.

Inaelezwa kuwa siku moja kabla ya tarehe husika kufika Simba walipigiwa simu na kusema kuwa wataweka fedha hizo lakini tarehe ilifika na Simba ikawa haijafanya malipo.

Baada ya muda kupita Simba ilianza kufanya malipo kidogo kidogo lakini Coastal waliandika barua ya kusitisha dili hilo kisha wakawarudisha Simba fedha zao zote walizowawekea.

Taarifa za uhakika zinasema kwamba Mchezaji alikula kiasi cha Tsh Milioni 130, huku pesa iliyobaki ilichukua klabu yake.

Hadi sasa bado mvutano unaendelea huku kwa upande wa Uongozi wa Simba kupitia kwa mshauri wa muwekezaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,  Mohammed Dewji, ndugu Crescentius Magori alisema;

“Simba tumewalipa kila kitu, na ushahidi wote tunao, hivyo kama klabu tupo sahihi hata waende FIFA”

Mchezaji Lameck Lawi inasemekana baada ya kusajiliwa na Simba, Uongozi wa Coastal Union ulipata ofa kubwa zaidi kutoka timu moja ya Ulaya, huenda waliingia tamaa ya kutaka kusitisha biashara na imba ili wafanya na klabu ya Ulaya, lakini bahati mbaya walikuwa wameshachelewa.

SOMA NA HII  MZEE WA KALIUA OSCAR: WATU WATAKULA SANA 5G...YANGA YA CHAMA NA GAMONDI