Home Habari za Simba Leo MFAHAMU KWA UNDANI DKT KAILIMA JUMBE MPYA WA SIMBA

MFAHAMU KWA UNDANI DKT KAILIMA JUMBE MPYA WA SIMBA

HABARI ZA SIMBA

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Ally Mangungu amemteua, Dr. Kailima Ramadhani Kombwey kuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Company Limited.

Taarifa ya Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo imebainisha kuwa Dkt. Kailima ataungana na wajumbe wengine waliochaguliwa kuiwakilisha Simba Sports Club katika bodi ya Wakurugenzi, sambamba na wajumbe wengine walioteuliwa na Muwekezaji, Mohammed Dewji.

“Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Ibara ya 27 (1) (d) ya Katiba ya Simba Sports Club, 2018 (Kama ilivyofanyiwa mare kebisho 2024) inayompa mamlaka Mwenyekiti wa Klabu kuteua wajumbe wawili wa bodi. Uteuzi huu unaanza kazi mara moja.”

Simba inaendelea kujipanga upya, baada ya kupoteana kwa misimu mitatu mfululizo, na tayari Bodi ya wakurugenzi upande wa mwekezaji Mo Dewji tayari imekamilika.

Kilichikuwa kimebakia ni upande wa wanachama kukamilisha nafasi zao, ili mchakato mzima wa kuiboresha Simba ianze.

Mashabiki wengi na wanachama ka upande wao, wamepokea taarifa hii ya uteuzi a Dkt Kailima kwa utofauti wake, wengi hawamfahamu ni mtu gani.

Lakini kwa ufupi tu Dkt Kailima aliwahi kupitia kwenye chama cha Mapinduzi kwa nafasi tofauti, wakiwa na rafiki yake Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba ambyae kwa upande wake ni Mjumbe wa Wadhamini wa Yanga.

Pia Dk. Kailima Ramadhani Kombwey kwa sasa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ambaye aliteuliwa Februari mwaka jana na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan akichukua nafasi ya Dk. Wilson Mahera Charles aliyehamishiwa kwenye nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

SOMA NA HII  BEKI KISIKI WA SIMBA APIGWA STOP KONGO