Home Habari za Simba Leo AHMED ALLY AWATULIZA MASHABIKI…ATAJA SIKU YA KUANZA KUTAMBULISHA

AHMED ALLY AWATULIZA MASHABIKI…ATAJA SIKU YA KUANZA KUTAMBULISHA

Habari za Simba SC

MENEJA wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema kuwa Kwa mipango yao ya usajili waliyopanga, basi nchi itasimama watakapoanza kutambulisha majembe yao waliyoyasajili msimu huu.

Akizungumzia usajili wa Simba Ahmed Ally alisema hawatakuwa na muda wa kufanya makosa tena, kwani kilichowatokea kwenye misimu mitatu mfululizo kimewapa funzo kubwa.

“Tumeteseka vya kutosha, misimu mitatu ya kukosa Ubingwa umetupa funzo kubwa mno, mipango ya usajili tuliyopanga nchi hii itatikisika.

“Msimu ujao wa mashindano 2024-25 kuna watu watakufa kutokana na wasiwasi wa maisha kwa ambacho watakifanya kwa mashabiki zao ambao wamekuwa na kiu ya kuona ubora wa timu hiyo unarejea,” alisema Ahmed Ally.

“Tunaendelea kutoa Thank You kwanza, tukimaliza tutaanza kutambulisha vyuma sasa, kuna huyo mchezaji anakimbia kama treni ya SGR”

Simba hadi sasa imewaacha wachezaji wanne wa klabu hiyo, Kuna John Bocco, Saidoo Ntibazonkiza, Shaban Iddy Chilunda, Luis Miquissone.

Moja kati ya jina yaliyotikisa sana baada ya Thank You, ni Luis Miquissone ambaye kuna baadhi ya mashabiki wanaona bado alikuwa anahitaji kupewa muda wa kuonesha kiwango chake kile.

Mkataba wa Miquissone ulikuwa bado haujaisha, alibakiza mwaka mmoja amalize mkataba na Simba, lakini klabu hiyo imeamua kumvunjia mkataba wake, ili kutoa nafasi ya kusaili wachezaji wengine.

Ni mchezaji aliyekuwa analipwa vizuri zaidi klabuni hapo, alikuwa anapokea kibunda cha dola 200,000/= sawa na zaidi ya Tsh Milioni 47.

Kwa kitita hicho cha pesa Simba wanaweza kusajili hata wachezaji wawili, wenye uwezo mkubwa zaidi ya Miquissone.

SOMA NA HII  MAMELODI SUNDOWN YAWAITA SIMBA SAUZI....WAANDAA MASHINDANO YAO KWA KLABU NNE TU ZA AFRIKA...