Home Habari za Simba Leo SIMBA WAKUBALI KUPITIA MAGUMU…WANAJIPANGA UPYA

SIMBA WAKUBALI KUPITIA MAGUMU…WANAJIPANGA UPYA

Habari za Simba Leo

HABARI ZA SIMBA LEO, Uongozi wa klabu hiyo imesikitishwa na kupoteza maombe muhimu msimu huuu, na kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea kwa msimu wa 2023/24

Simba ilidhamiria kuchukua ubingwa wa Ligi kuu NBC, FA, na kufika nusu fainali Ligi  ya mabingwa,  lakini hakuna hata moja walilopata zaidi ya kuambulia nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu.

Kombe la Shirikisho la CRDB wamepishana nalo kwa misimu mitatu sasa, tangu wafanye hivyo mara ya msimu wa 2020/21.

Ule ukuta wa Simba SC WENYE Che Malone baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 uliruhusu mabao 25 na safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 59.

Wakati Simba ikishuhudia taji la ligi likiwa mikononi mwa Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika iligotea hatua ya robo fainali ikikwama kutwaa taji hilo kubwa Afrika na iliposhiriki African Football Cup iligotea hatua ya robo fainali.

Simba ni mashuhuda wa bingwa mpya wa CRDB Federation Cup kuwa ni Yanga iliyoshinda kwa penalti 6-5 dhidi ya Azam FC kwenye fainali iliyochezwa Juni 2 2024, Uwanja wa New Amaan Complex.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa ulikuwa ni msimu wenye ushindani mkubwa na matarajio yao yote hayajatimia jambo linalowapa masikitiko.

“Tuna majonzi makubwa kwa wakati huu ninatambua kwamba Wanasimba hawajafurahi namna ambavyo tumamaliza, haya ni masikitiko kwetu hatujafikia malengo yetu kwa asilimia kubwa hilo lipo wazi.

Nyakati zinabadilika hivyo tunaamini kwamba tutarejea tukiwa imara.

“Bado tuna muda wakufanyia kazi makosa ambayo yalipita kwa ajili ya kuwa imara wakati ujao, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi mambo mazuri yanakuja na tutafanya vizuri katika wakati ujao.”

SOMA NA HII  MAXI MZUKA KIBAO KUELEKEA DABI YA KARIAKOO