Home Habari za Simba Leo UKIMYA WA SIMBA…WAMUIBUA AHMED ALLY…ASEMA JAMBO

UKIMYA WA SIMBA…WAMUIBUA AHMED ALLY…ASEMA JAMBO

Habari za Simba leo

HUENDA hata wewe umekuwa ukipita kwenye akaunti mbalimbali za klabu ya Simba  kujaribu kuchungula taarifa mpya, lakini huoni chochote! ukimya huo umemfanya Afisa Habari wa Klabu hiyo kuibuka na kutoa neno kwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo.

Ahmed Ally amewasihi mashabiki wa na wanachama wa klabu ya Simba watulie mambo mazuri yanakuja.

“Wiki moja tangu ligi imalizike na kumekua na ukimya wa taarifa kutoka Simba Sports Club kiasi cha kuzua hofu kidogo”

“Usahihi ni kwamba mipango na mikakati thabiti inaendelea na itakapokua tayari Wana Simba wote mtajulishwa.

“Jambo la kufurahisha ni kwamba mipango yote inatekelezwa kwa ustadi na ufanisi wa hali ya juu mnoo.

“Malengo tuliyojiwekea ya kuboresha timu yetu yamefikiwa kwa asilimia kubwa kwa maana ya kwamba mipango yetu kwenye soko la usajili iko vizuri sana

“Niwaombe Wana Simba tutulie, la mgambo likilia tutafahamu kila kitu kuhusu timi yetu pendwa”

Kauli ya Ahmed Ally inakuja baada ya kuwepo kwa taarifa nyingi za usajili kuihusu klabu hiyo, moja ya sajili zinazopewa nafasi kubwa hapo ni majina haya ya wachezaji.

Winga wa kushoto Elie Mpanzu kutoka AS Vita, Steve Dese Mukwala anakipiga Asante Kotoko, na kiungo wa timu ya taifa ya Uganda aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya SC Villa Kenneth Semakula, Yusuph Kagoma, Lameck Lawi.

SOMA NA HII  STAA HUYU WA SIMBA ANAJUTA KUONDOKA YANGA, STORI KAMILI IKO HIVI