Home Habari za Simba Leo AHMED ALLY AFUNGUKA DILI LA MPANZU LILIPOFIKIA

AHMED ALLY AFUNGUKA DILI LA MPANZU LILIPOFIKIA

Habari za Simba- Mpanzu

MENEJA wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amevunja ukimya na kukiri kuwa wamerudi kwa mara nyingine zaidi kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa AS Vita ya DR Congo, Elie Mpanzu.

Amesema Mpanzu ni mchezaji wa kwanza aliyependekezwa katika usajili wa Simba lakini kutokana na ugumu umechelewesha hadi sasa wamekuwa wanaingia na kutoka katika la nyota huyo.

Imeelezwa kuwa Simba walikuwa wametuma ofa ya dola 200,000 sawa na million 540, huku klabu ya nyota huyo ikihitaji dola 250,000, kwa sasa Simba wameongeza dau na kwenda 225,000 sawa na Milioni 607.

Wakati Simba wakisubiri majiba kutoka As Vita, nyota huyo hajajiunga na timu yake hiyo iliyoanza maandalizi ya msimu mpya na inadaiwa amepata mwaliko wa kwenda klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji kwa ajili ya Majaribio.

Ahmed amesema wamepeleka ofa yao ndani ya klabu hiyo waliweka ugumu na baadae wakaacha nayo lakini sasa hivi hilo suala lipo na kutoka.

Amesema viongozi wamekuwa wakifatilia kuhakikisha wanafanikiwa kunasa saini ya kiungo mshambuliaji huyo kwenda kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa ajili ya msimu ujao.

“Kweli Mpanzu ni mchezaji mzuri suala lake lipo 50 kwa 50, inaenda na kurudi, awali tulifatilia ikawa ngumu na sasa tumerejea kuangalia kama tutaweza kupata huduma yake,” amesema Meneja huyo wa simba.

Kuhusu kumfatilia Mpanzu ni kwa ajili ya mbadala wa mshambuliaji wao, Kibe Denis, Ahmed amesema suala la nyota huyo limefika kwa mwanasheria wa Simba, kupokea barua kutoka klabu ya Kristiansund Bk ya nchini Norway.

Dili la Mpanzu kusajiliwa na Simba likifanikiwa kuna baadhi ya wachezaji wa kigeni wanalazimika kupewa ‘THANK YOU’, huku akidaiwa Fredy Michael.

SOMA NA HII  FERNANDES MAVAMBO APEWA MZIGO MKUBWA SIMBA