Home Habari za Simba Leo ALIYEGOMEA MKATABA YANGA…ATAMBULISHWA SIMBA

ALIYEGOMEA MKATABA YANGA…ATAMBULISHWA SIMBA

HABARI ZA SIMBA-YUSUPH KAGOMA

KLABU YA Simba SC Imetangaza kuinasa saini ya Kiungo wa Ulinzi Yusuph Kagoma (28) kwa mkataba wa miaka mitatu hadi msimu wa 2026/2027.

Awali mchezaji huyo alikuwa anahusishwa zaidi na watani zaoYanga, kabla ya upepo kubadilika na kijana huyo kusaini mkataba na Simba, hali ya kuwa tayari alikuwa kishasinya mkataba wa awali na Yanga.

Inasemekana kwamba Dau kubwa la pesa lililowekwa na Simba, ndio lilimvutia zaidi Kagoma, hadi kuoma kusaini mkataba rasmi na Yanga na kuwaomba Viongozi wake wa Singida Fountain Gate kurudisha pesa za Yanga.

Sehemu ya Taarifa ya Simba kutoka Simba App iliandika kwamba, Kagoma ni seemu ya mpango wa Simba kurudisha ubora wao.

“Kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma ni mchezaji wetu mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu ya kukitumikia kikosi chetu kutoka Singida Fountain Gate.”

“Kagoma ni moja ya vijana wazawa wenye uwezo mkubwa wa kuzuia timu ikishambuliwa na kupandisha mashambulizi.”

“Uwezo wake na umri wake ni miongoni mwa vigezo vilivyotuvutia kutafuta saini yake na tuna matarajio makubwa kutoka kwake.”

“Kagoma yupo kwenye mipango ya maboresho makubwa ya kuirejesha timu katika ubora ambao mashabiki wetu wanatamani kuiona.”

Baada ya kukamilika kwa usajili huu wa Yusuph Kagoma, sasa safu ya Viungo ya Simba inakuwa na wachezaji 6, ikiongozwa na Mzawa Mzamiru Yassin, Fabrice Ngoma, usajili mpya ni Augustine Okejepha kutoka Rivers Utd, Deborah Fernandes, Jean Charles Ahoua na YUsuph Kagoma.

Simba inatarajiwa kuanza safari ya kuelekea Misri kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25.

SOMA NA HII  SIRI YA USHINDI WA YANGA UGENINI IKO HAPA