Home Habari za Simba Leo ELIE MPANZU AFUNGUKA KUHUSU SIMBA…AITAJA KRC GENK

ELIE MPANZU AFUNGUKA KUHUSU SIMBA…AITAJA KRC GENK

Habari za Simba- Mpanzu

BAADA ya Simba kurudi kwa mara ya tatu kujaribu kuinasa saini ya Winga wa AS Vita Elie Mpanzu, lakini bado mambo yameonekana kuwa magumu baada ya mchezaji mwenyewe kufunguka kila  kitu.

Simba inamuhitaji sana Elie Mpanzu, lakini dau lililowekwa na klabu hiyo ya kutaka Dola 250,000 (zaidi ya Sh 500 milioni) kumuachia liliwazuia Msimbazi kumbeba mapema kama ilivyofanya kwa nyota wengine waliopo kambini Misri.

Simba ilikuwa ikimuona Mpanzu kama mbadala sahihi wa Kibu kama atapata timu nje kutokana na aina yao ya kiuchezaji, wakiwa na kasi, nguvu na kutochoka haraka uwanjani mbali na kusaidia kukaba.

Kwa mujibu wa Gazeti la Mwanaspoti ni kwamba Mpanzu mwenyewe kfaunguka ukweli wa kufuatwa na Simba na kuweka bayana kwa kutoa msimamo alionao, akiitaja klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji aliyowahi kuitumikia Mbwana Samatta

Mpanzu alisema ni kweli Simba imekuwa ikimtaka na ilikuwa ikifanya mazungumzo na mabosi wa AS Vita, lakini msimamo wake ni kwenda kucheza soka Ulaya na sio Msimbazi.

Mpanzu alifichua sababu hasa ya msimamo huo wa kuikacha Simba na kutaka kwenda Ubelgiji kukipiga Genk ni familia yake sambamba na ndoto za muda mrefu alizonazo za kucheza Ulaya.

“Familia ilinishauri kuishi katika ndoto zangu na sio kuangalia maslahi kila wakati, hiyo tu imekuwa sababu yenye nguvu sana moyoni mwangu, kwani nataka kufanya kazi kwa furaha,” alisema Mpanzu na kuongeza;

“Nilitaka kuja Simba kwani nayo ni timu kubwa na nzuri, lakini kuna wakati nilitakiwa kufikiria mbele zaidi kwani hata kama ningekuja huko bado ningekuwa naiwaza ndoto yangu ya kuchezea Ulaya.”

Simba ilikuwa tayari imeshakubaliana na Mpanzu kusaini mkataba wa miaka miwili, lakini baadaye vigogo wanaommiliki winga huyo akiwemo Rais wa AS Vita Amadou Diaby, aliingilia kati dili hilo na kumzuia staa huyo kusaini kwa kutaka dau nono zaidi na ndilo lililowarudisha nyuma vigogo wa Msimbazi.

Kutokuja kwa Mpanzu ndani ya Simba kumewapa shavu Willy Onana na Freddy Koublan kusalia Msimbazi, kwani awali mmoja ilikuwa lazima ampishe Mkongomani huyo, huku ikielezwa Onana alikuwa na nafasi kubwa kwa vile kuna ofa kutoka Qatar.

SOMA NA HII  BENCHIKA AIFANYIA SIMBA UMAFIA...ACHUKUA WAWILI HOFU YATANDA.