Home Habari za Simba Leo KAPOMBE & ABEL WATAJA UGUMU WA SIMBA YA SASA

KAPOMBE & ABEL WATAJA UGUMU WA SIMBA YA SASA

Habari za Simba- Hussein Abel

KIPA wa Simba, Hussein Abel amesema kwa aina ya mazoezi yanayofanywa na kikosi hicho yanampa taswira ya jinsi ambavyo watakuwa na ushindani dhidi ya wapinzani wao.

Akizungumza baada ya ushindi katika mechi ya kirafiki dhidi ya El Qanah ya Misri mjini Ismaili kwa mabao 3-0, Abel amesema: “Ushindani unaanzia mazoezini kila mchezaji anatamani kuona kocha anaona uwezo wake. Hilo linanipa nguvu ya kuona Simba itafanya makubwa msimu ujao.

“Jambo la msingi ni mashabiki kutuunga mkono ili kufanya vitu vikubwa kwa umoja, tutafikia malengo yetu.”

Awali, beki wa timu hiyo, Shomari Kapombe amesema kuna kitu kikubwa anakitengeneza kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids kitakachowasaidia kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya msimu ujao.

Kapombe amesema kocha huyo amekuwa akiwajenga katika mazoezi ya stamina, ufiti na akili kuwaza ushindi, jambo ambalo limewafanya washinde mechi hiyo.

“Tumekuwa na wakati mzuri katika kambi yetu, kocha anatupa vitu vikubwa kiufundi, tumejikuta kila mchezaji ana morali ya kufanya kazi, imani yangu ni kubwa kwamba msimu ujao utakuwa wa mafanikio kwetu,” amesema.

Ameongeza: “Ongezeko la wachezaji wapya katika timu, umekuwa na manufaa makubwa, wana vipaji vikubwa ni vijana ambao wanatamani kujifunza zaidi na wana utayari wa kushika kila kitu ambacho kocha anakielekeza.”

Simba watacheza mchezo mwingine wa kirafiki kabla ya kusafiri kurudi nchini, kwaajili  ya Simba Day na mechi za Ngao ya Jamii ambapo mchezo wao wa nusu fainali watacheza na Yanga.

SOMA NA HII  SIMBA YATAMBA..... HUKU YANGA HALI SIO HALI U20