Home Habari za Simba Leo MANARA CHIMBA MKWALA…SIMBA ASILETE TIMU

MANARA CHIMBA MKWALA…SIMBA ASILETE TIMU

Habari za Yanga

Mhamasishaji wa  Klabu ya Yanga SC, Haji Manara amesema Simba SC wasiende Uwanjani Agosti 08 katika pambano lao Ngao ya Jamii la kuashiria kufunguliwa kwa msimu mpya.

Manara amesema wana timu imara na ya maana, hivyo mashabiki wa Simba SC wakaidi watakaoenda kiwanjani siku hiyo watakutana na maumivu.

“Tuna Chama, tuna Pacome. Tutaenda kuwafunga Simba SC si chini ya bao 4, tulikuwa na timu imara na timu ile imara imeongezewa watu wachache. Tuna kocha yule yule, wenzetu timu yao mpya. Jamani wasije Hajis Manara.

“Wachezaji kila ukiwauliza wanasema wao wanawaza Agosti 8 tu, nawaambia Simba SC wasilete timu yao uwanjani. Baleke ana hasira yani waambieni Agosti 08 wasilete timu uwanjani zile tano zisipojirudia sijui,” alisema Manara.

Simba na Yanga zinatarajiwa kucheza mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Ngao ya Jamii, mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana, Simba ilipoteza mchezo kwa mabao 2-1, huku mzunguko wa kwanza wa msimu  wa 2023/24 Simba ilichapwa 1-5.

SOMA NA HII  CHAMA MFUNGAJI BORA LIGI YA MABINGWA...LIST KAMILI HII HAPA