Home Habari za Simba Leo BENO KAKOLANYA ASIMULIA MECHI YAKE YA KWANZA

BENO KAKOLANYA ASIMULIA MECHI YAKE YA KWANZA

HABARI ZA SIMBA-KAKOLANYA

Kipa wa zamani wa Simba na Yanga Beno Kakolanya kwa sasa anakipiga na wauaji wa Kusini Namungo FC, amesema kuanza kwao vibaya mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Tabora United iliyowafunga mabao 2-0, imewafungua macho kukaza buti.

Alisema Tabora United ilikuwa na kikosi cha wachezaji wazuri kama mshambuliaji Heritier Makambo, hivyo ushindani ulikuwa mkubwa ambao uliwapa wapinzani wao ushindi.

“Hakuna kitu kibaya kama kufungwa nyumbani, lakini imetuamsha kukaza buti zaidi. Msimu umeanza na kasi kubwa, inaonyesha jinsi Ligi Kuu itakavyokuwa ya ushindani,” alisema.

“Kwa sasa tunaweka nguvu dhidi ya Fountain Gate baada ya awali kuahirishwa mechi hiyo, kwani wachezaji wao walikuwa hawana vibali. Wapinzani wetu nao wamepoteza dhidi ya Simba kwa mabao 4-0, hivyo utakuwa mchezo mgumu.”

Kakolanya anakwenda kukutana na timu yake ya zamani (Fountain Gate), alisema kitu kinachotakiwa kwenye mchezo huo ni ushindi na siyo kupoteza.

“Hatutaki kung’ang’aniwa na gundu la kupoteza tena, ila tupate morali na kuambulia pointi iwe moja ama tatu,” alisema

SOMA NA HII  YANGA YATUMA SALAM KWA KINO BOYS