Home Habari za michezo CAF WAIPIGA YANGA ‘STOP’ KWENDA ZNZ….ISHU KAMILI IKO HIVI…

CAF WAIPIGA YANGA ‘STOP’ KWENDA ZNZ….ISHU KAMILI IKO HIVI…

Yanga SC

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) wazuia Uwanja wa Amaan Complex kutumika kwenye mchezo wa Yanga SC wa Klabu Bingwa Barani Afrika.

Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said amesema kuwa wameomba uwanja wa Amaan Zanzibar kwa ajili ya mechi ya raundi ya pili ya mtoano dhidi ya CBE FC ya Ethiopia.

“Moja kati ya vigezo vya uwanja sio tu sehemu ya kuchezea au ubora ila ni pamoja na umbali wa viti kutoka kimoja hadi kingine, kwa uwanja wa Amaan umekosa ivyo vigezo.

“Uwanja kama wa Azam Complex unakidhi vigezo kutokana na umbali wa viti ambao kwa vigezo vya CAF wanataka kuanzia sentimita 45.

“Azam walilazimika kupunguza idadi ya namba ya mashabiki kutoka elfu 6 hadi elfu 4 ili kukidhi vigezo vya CA,F” amesema Mchambuzi wa Soka, Geoff Lea.

SOMA NA HII  OHOO KUMBE SKUDU ANAJAMBO LAKE NA GAMONDI...... ISHU NZIMA IKO HIVI