Home Habari za Simba Leo FREDDY MICHAEL ATUPA DONGO SIMBA.

FREDDY MICHAEL ATUPA DONGO SIMBA.

HABARI ZA SIMBA-fREDDY

SAA chache baada ya kutemwa na Simba, mshambuliaji Freddy Michael amevunja ukimya na kufunguka akisema alichofanyiwa imekuwa ni kama sapraizi kwani alikuwa amejipanga kufanya makubwa baada ya kujipata mwishoni mwa msimu uliopita.

Freddy Michael ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Green Eagles ya Zambia, amesema licha ya kuwaheshimu na kuwakubali mastraika wapya waliotua Msimbazi, lakini amewaponda kwamba hakuna yeyote wa kumfikia kwa kazi ya kufunga, hata kama alianza na mguu mbaya aliposajiliwa katika dirisha dogo la msimu uliopita.

“Imenishtua mno, kwani malengo niliyokuwa nayo msimu huu ilikuwa ni kufika mbali hata kubeba kiatu cha mfungaji bora, kwa vile nilishaizoea ligi ilivyo na hata namna ya kucheza. Nilihitaji mechi nyingi tu, kuonyesha kile nilichokuwa nacho kwa kuwa, sikuwa na kiwango kibaya msimu uliopita ndio maana nilimaliza na mabao mengi kuwazidi waliocheza kwa msimu mzima,”

“Nawaheshimu washambuliaji waliobaki Simba, lakini nilikuwa na uwezo wa kufanya kitu bora kuliko wao, najua kipaji changu na wenyewe mliona nilivyoizoea ligi. Hata hivyo kwa sasa nasubiri kumalizana na timu moja kwenda kuendeleza ubora wangu huko.” Amesema Freddy..

Simba imeachana na nyota huyo wa Ivory Coast, baada ya kudumu kwa miezi takribani 8, huku akicheza mechi 13 za Ligi Kuu akiwa na Simba, na kufanikiwa kufunga mabao 6.

Ujio wa Leonel Ateba ni sababu ya kwanza ya kumuondoa Freddy Unyama, hii ni kwa sababu ya idadi ya wachezaji wa Kimataifa kukamilika.

Na sasa mchezaji huyo amejiunga na klabu ya Algeria USM Alger, ambayo ametokea mshambuliaji mpya wa Simba Leonel Ateba.

SOMA NA HII  KAKOLANYA AWASALITI SIMBA...AWEKEWA DONGE NONO...AMESAJILIWA NA TIMU HII