Home Habari za Simba Leo JOSHUA MUTALE AWAITA MASHABIKI TAREHE 8…AAHIDI KUWAPA FURAHA

JOSHUA MUTALE AWAITA MASHABIKI TAREHE 8…AAHIDI KUWAPA FURAHA

HABARI ZA SIMBA- mUTALE

Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya APR ya Rwanda, katika Tamasha la Simba Day, winga mchachari wa timu hiyo, Mzambia, Joshua Mutale, amesema wamesahau hilo na sasa akili na nguvu zote wanazielekeza katika mechi inayofuata dhidi ya Yanga.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Joshua Mutale, mmoja wa wachezaji wapya, waliosajiliwa msimu huu akitokea Power Dynamos ya Zambia, alisema baada ya kupata ushindi huo, wamekuwa na ari na kujiamini kiasi cha kutaka kuendeleza ushindi katika mechi ijayo ili kuwapa furaha mashabiki wao ambao walijitokeza kwa wingi Jumamosi kuwasapoti.

“Tumewaonyesha mashabiki ni kitu gani tunataka kufanya kuelekea msimu ujao, kizuri ni kwamba tumeanza kilele cha Simba Day kwa ushindi, na sasa tunaangalia mechi inayofuata dhidi ya Yanga, tunajiandaa na hilo na tutapambana,” alisema winga huyo ambaye alionesha kiwango kikubwa katika mchezo huo.

Mchezaji huyo ameonesha kushangazwa na umati mkubwa uliojitokeza akisema ni kitu cha ajabu sana kukiona kwa macho.

“Ni kitu cha ajabu sana kwangu hiki nilichokiona, umati mkubwa kama ule, ulitufanya wachezaji kupambana uwanjani, kwangu ilikuwa ni mechi ya kwanza kubwa ya aina yake nikiwa na Simba,” alisema Mutale.

SOMA NA HII  MAMA SAMIA:- SIMBA NA YANGA WEKENI MAGOLI NYAVUNI...MIL TANO TANO BADO ZIMEJAA