Home Habari za Simba Leo MAINGIZO MAPYA SIMBA NA YANGA…UBORA WAO

MAINGIZO MAPYA SIMBA NA YANGA…UBORA WAO

Habari za Simba na Yanga

Katika maboresho ambayo Simba na Yanga imefanya katika dirisha hili la usajili, wapo wachezaji ambao tayari wameanza kuonyesha makali yao na huenda wakaongeza makali ya vikosi hivyo.

Beki wa kati Chamou Karaboue; viungo Joshua Mutale, Debora Mavambo, Jean Charles Ahoua, Augustine Okejepha na Awesu Awesu hao ni baadhi ya nyota wapya kwa Simba ambao wameanza kuonyesha makali yao katika michezo minne waliyocheza ya kirafiki.

Viwango vya wachezaji hao vimebeba matumani ya mashabiki wa Simba katika safari mpya ya ujenzi wa kikosi chao.

Tofauti na Simba, Yanga imefanya maingizo machache ambayo yanaonekana ni kama mwarobaini hasa katika maeneo ambayo walionekana kuwa na mapungufu msimu uliopita.

Usajili wa Prince Dube, Jean Baleke umeonekana kuwa na matumaini kwa Yanga katika safu yao ya ushambuliaji kutokana na walichokifanya washambuliaji hao katika michezo ya kirafiki.

Duke Abuya ameonyesha kuna kitu anaweza kukiongeza kwenye kikosi cha Yanga tofauti na Clatous Chama ambaye bado anajitafuta, eneo lingine ambalo Yanga imelifanyia maboresho ni beki ya kushoto na Chadrack Boka ameanza kuonyesha makali yake.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA INAVYOCHEZA...ADEBAYOR AZIDI KUFUNGUKA HAYA KUHUSU SIMBA...