Home Habari za Simba Leo MZIMU WA MIGOGORO SIMBA WARUDI…ZAMU YA VALENTINO

MZIMU WA MIGOGORO SIMBA WARUDI…ZAMU YA VALENTINO

habari za simba-Mashaka

SIMBA ni kama kuna harufu mbaya inazunguka pale mitaa ya Msimbazi kutokana na migogoro ya wachezaji wa ndani.

Mjadala ulanza kwa mchezaji Lameck Lawi, ukaja kwa kwa Yusuph Kagoma baadae akaja Awesu Awesu, na sasa sakata hilo limefika kwa Mshambuliaji wa klabu hiyo.

Mchambuzi wa michezo kituo cha habari cha Clouds FM, Farhan Kihamu aliandika haya;

Kwenye yale mapingamizi matatu ya Wachezaji wa Simba ambao wamewekewa kutoka kwenye klabu tatu, pingamizi moja linafurahisha sana.

Licha ya kuwa mkataba unasema wazi Simba wapo sahihi ila klabu iliyokuwa inamiliki Mchezaji inasema Simba walipaswa kuwataarifu angalau na sio tu kumalizana na Mchezaji juu kwa juu yani wao walitaka Simba itambue uwepo wao, duru zikiarifu kuwa ni Geita Gold hao kwa Valentino Mashaka.

Sasa kutokana na Simba kutotambua uwepo wao, Simba wamepata ugumu kupata leseni ya Mchezaji maana kila wakiomba kwenye mfumo (TMS) wao wanakataa kuachia ili Mchezaji aingie kwenye mfumo wa Simba, maana mchakato ni kuwa Mchezaji unamwomba kwenye mfumo na Klabu mmiliki ndio inapaswa kumrelease ila wao wamekaza.

Sakati la Mchezaji mwingine kutoka KMC wao wanadai mzigo sio MILLION 50 za Awesu bali ni MILLION 70 kwahiyo ndio vurugu zipo hapo kati.

SOMA NA HII  RASMII....BAADA YA KUNGOJEANA SAAANA...HATIMAYE MOSES PHIRI AANZA KUKIWASHA NDANI YA SIMBA...MAVITU YAKE BALAA..