Home Habari za Simba Leo SIMBA YAFANANISHWA NA BARCA YA XAVI & INIESTA WENGINE R.MADRID

SIMBA YAFANANISHWA NA BARCA YA XAVI & INIESTA WENGINE R.MADRID

Habari za Simba

MASHABIKI wa Simba, akiwemo mdau mkubwa wa timu hiyo Mohammed Soloka amesema mwitikio mkubwa wa mashabiki wa timu hiyo kujaza Uwanja wa Mkapa ni kielelezo cha kiu yao kutaka kuiona timu yao mpya.

Soloka amesema mashabiki wenzake wengi wamefurahishwa na namna uongozi wa klabu hiyo ulivyojenga kikosi kipya chenye wachezaji wengi vijana.

Kigogo huyo amesema wachezaji waliosajiliwa ni wenye vipaji vikubwa wasio na majina makubwa, sera ambayo inatumika hata Real Madrid ya Hispania.

“Watu wamefurahishwa na usajili ulivyofanyika wakati huu, tumekuwa na timu ya wachezaji vijana wasio na majina makubwa. Hii ni sera inayotumika hata kwa Real Madrid ya Hispania ambao ni Mabingwa wa Ulaya,” amesema Soloka.

“Tumekuja kuwaona wachezaji wetu, ndio maana unaona tumeujaza uwanja kwa haraka. Tunaamini kwamba wataturudishia heshima iliyopotea kwa miaka mitatu Sasa.”

SOMA NA HII  SILAHA HATARI YA SIMBA YAREJEA...MSIMBAZI WAZIDI KUJIKOKI...HOROYA WATAKIMBIA