Home Habari za Simba Leo MANULA, ONANA WAPEWA THANK YOU SIMBA.

MANULA, ONANA WAPEWA THANK YOU SIMBA.

habari za simba

ALIYEKUWA kipa namba moja wa Simba, Ashi Manula ametemwa kwenye kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao wa 2024/25 baada ya timu hiyo kutambulisha makipa wanne huku jina lake likiondolewa.

Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ndiye alikuwa anataja majina ya mastaa wa kikosi hicho msimu ujao katika tamasha la Simba Day linalofanyika Uwanja wa Mkapa, ambapo ametaja majina manne eneo la makipa.

Makipa hao ni Ally Salim, Ayoub Lakred, Mohammed Camara na Hussein Abel ndiyo idadi ya walinda lango  watakaoiongoza Simba eneo la golini.

Wakati wa kutaja majina hayo nyomi ya mashabiki iliyojaza uwanja iliibua shangwe baada ya kusikia jina la Lakred ambaye inaelezwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kutokana na kuumia akiwa mazoezini.

Pia shangwe kubwa limeibuka baada ya kutajwa kwa kipa mpya wa timu hiyo ambaye amesajiliwa kwa lengo la kuziba pengo la Lakred ambaye atakuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza jeraha alilolipata.

“Hawa ndio walinda mlango ambao tutakuwa nao msimu ujao,” amesema Ahmed.

Jina la Mchezaji mwingine ambaye ni moja kwa moja amepewa Thank You ni Willy Essomb Onana, baada ya jezi yake namba 7 kuvaliwa na Joshua Mutale.

Onana inaelezwa amepata timu moja ya nje ya Afrika na tayari amefikia makubaliano na klabu hiyo.

SOMA NA HII  KAMBI YA YANGA IMENOGA...AUCHO NA DIARRA WAONGEZA MZUKA