Home Habari za Simba Leo SIMBA YAMUAGA KAJULA…REGIS FRANCOIS ATAMBULISHWA

SIMBA YAMUAGA KAJULA…REGIS FRANCOIS ATAMBULISHWA

Imani Kajula CEO mpya wa Simba

ALIYEKUWA CEO wa Simba, Imani Kajula ameagwa rasmi jana kwenye kilele cha tamasha la Simba Day linalofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kajula alijiunga na Simba mwaka 2022 na aliwahi kuwa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Masoko na Mawasiliano ya EAG Group tangu 2013 hadi 2023 ambapo ataondoka rasmi ndani ya kikosi hicho Agosti 31, mwaka huu.

Ofisa mtendaji huyo alichukua nafasi iliyoachwa na Barbara Gonzalez ambaye alijiuzulu nafasi hiyo ndani ya kikosi hicho Desemba 10, 2022.

Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alitangaza kumuaga kwa kiongozi huyo na kisha kumtambulisha mtendaji mpya, Uwayezu Francois Regis, raia wa Rwanda.

“Rasmi tunamuaga aliyekuwa mtendaji wetu, Imani Kajula baada ya kumaliza mkataba nasi mwezi huu. Tunamshukuru kwa kipindi chote alichohudumu. Wakati tunamuaga, tutumie wakati huu kumtambulisha mkurugenzi mpya, Regis,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  KOCHA AFUNGUKA HAYA BAADA YA MANULA KUREJEA KIKOSINI