Home Habari za Simba Leo RAIS SAMIA AWASHAUI SIMBA HAYA…TUGANGE YAJAYO…

RAIS SAMIA AWASHAUI SIMBA HAYA…TUGANGE YAJAYO…

Habari za Simba

RAIS wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Simba kwa kufanikisha kuandaa tamasha la Simba Day, Jana Agosti 3.

Tamasha hilo  ni la 15 tangu kuanzishwa  kwake na Field Marshall Mzee Hassan Dalali ambaye alikuwa Mwenyekiti wa klabu y Simba.

Rais Samia alituma salamu zake na pongeza kwa klabu hiyo huku akiwa ujumbe wa yaliyopita sio ndwele, wagange yajayo.

“Hongera Simba na Wanasimba kwa kufanikisha Simba Day 2024. Nawatakia kila la kheri katika msimu mpya wa Ligi Kuu. Waswahili wanasema, yaliyopita si ndwele”. -Rais Samia Suluhu Hassan.

Mashabiki wengine wa Simba waliongelea kiwango cha timu yao,  baada ya kuiona kwa mara ya kwanza ikicheza jana  dhidi ya APR ya Rwanda na kushinda mabao 2-0,

Mabao hayo yalifungwa na kiungo fundi “Disconnector” Debora Fernandes Mavambo na Edwin Balua yote katika kipindi cha pili.

“Watu wamefurahishwa na usajili ulivyofanyika wakati huu, tumekuwa na timu ya wachezaji vijana wasio na majina makubwa. Hii ni sera inayotumika hata kwa Real Madrid ya Hispania ambao ni Mabingwa wa Ulaya,” amesema Soloka.

“Tumekuja kuwaona wachezaji wetu, ndio maana unaona tumeujaza uwanja kwa haraka. Tunaamini kwamba wataturudishia heshima iliyopotea kwa miaka mitatu Sasa.”

Soloka ambaye ni mtendaji Mkuu wa kampuni ya Silent Ocean, ameongeza kuwa timu hiyo imefanya uamuzi mzuri na mgumu kwa kuwaacha wachezaji wenye umri mkubwa bila kujali vipaji vyao.

SOMA NA HII  YALIYOMKUTA ACHRAF HAKIMI...YAMNYEMELEA C.RONALDO...ISHU NZIMA IKO HIVI