Home Habari za Simba Leo STRAIKA WA USM ALGER AHITAJIKA CHAP SIMBA

STRAIKA WA USM ALGER AHITAJIKA CHAP SIMBA

habari za simba-Ateba

INAELEZWA kwamba Simba SC wako karibu na kumsajili mshambuliaji wa kati kutoka Cameroon, Leonel Ateba (25), yote yamehakikishwa.

Mchezaji huyo amevutiwa zaidi na Project ya Simba na yupo tayari kujiunga na Simba. Hakuna tatizo upande wake.

Kwa sasa, Simba na USMA wanafanya mazungumzo kuhusu ada ya uhamisho wa Ateba!

Awali, alicheza kwa Coton Sport, PWD Bamenda na Dyn. Douala na alijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 27 wa Cameroon kwa ajili ya AFCON 2023.

Simba imelazimika  kurudi sokoni  haraka  kutafuta mshambuliaji mwingine wa kumpa nguvu Steve Mukwala,  ambaye muda mwingi amekuwa akiteseka kwa kuwasumbua mabeki lakini Simba inakosa mshambuliaji mwingine wa kutumia  mipira inayoporwa na Mukwala.

Simba imecheza jumla  ya dakika 180 bila washambuliaji wake kufunga bao hata moja, huku kwenye mechi hizo 3 wakiwa wamefunga mabao 3 sawa na wastani wa goli 1 kwa kila mechi.

Ujio wa Ateba unaiweka mashakani nafasi ya mshambuliaji wa sasa wa timu  hiyo Fredy Michael Fungafunga.

SOMA NA HII  BREAKING NEWS...DILI LA KIBU DENIS LIMEKUFA RASMI...SIMBA WAMUITA DAR