Home Habari za Simba Leo TETESI ZA USAJILI…FREDDY FUNGA FUNGA ANAHITAJIKA TIMU YA ATEBA.

TETESI ZA USAJILI…FREDDY FUNGA FUNGA ANAHITAJIKA TIMU YA ATEBA.

habari za simba-Freddy

Huenda muda wowote kutoka sasa mshambuliaji wa Simba Freddy Michael Koublan akajiunga na USM Alger ya Ligi Kuu Algeria.

USM Alger wanataka kumsajili Fred kama mbadala wa Leonel Ateba aliyetimkia Simba SC.

Freddy licha ya kutua Simba dirisha dogo la usajili amefunga mabao 6 katika mechi zake 13 za Ligi kuu alizocheza. Kitakwimu namba zake ni nzuri na zina mbeba kuendelea kuwa moja ya wafungaji hatari.

Lakini kinachomuondoa Simba ni presha tu ya mashabiki kutaka kuendena na upepo wa majirani zao Yanga, ndio maana wameenda kusajili mchezaji mwingine ambaye msimu mzima amefunga bao moja tu.

Ateba huenda akawa na msaada pia kwa Simba, kama kocha mkuu wa klabu hiyo Fadlu Davids ataamua kumchezesha namba 9, tofauti na alipotoka alikuwa akicheza winga au namba 10, kwahiyo muda mwingi alikuwa anatengeneza magoli zaidi kuliko kufunga.

Kwa Freddy Michael Funga Funga atakapojiunga na USM Alger huenda akafanya makubwa zaidi kulingana na aina ya wachezaji waliopo huko, lakini pia presha ya timu anayoenda kuichezea hailingani na presha ya Simba kwa sasa ambao hawana ubingwa wa Ligi kuu kwa msimu wa 3 mfululizo.

SOMA NA HII  SIMBA IMEANZA KUJIPATA...SIKIA KUHUSU AWESU NA WENZAKE