Home Habari za Simba Leo WANASIMBA NJOONI MUONE SHOW YA KIBABE…AHMED ALLY AWAITA WANAMSIMBAZI

WANASIMBA NJOONI MUONE SHOW YA KIBABE…AHMED ALLY AWAITA WANAMSIMBAZI

Habari za Simba, Ahmed Ally

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa Wanasimba wasikubali kukaa nyumbani Agosti 31 2024 timu hiyo itakapokuwa ikicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids leo inatarajiwa kutupa kete hiyo ya kimataifa saa 10:00 jioni.

Ahmed Ally amebainisha kuwa ni mchezo mzuri utakaowapa furaha mashabiki wa Simba kwa kuwa wachezaji wanapenda kutimiza majukumu yao wakiwa uwanjani.

“Wanasimba ni mchezo wetu wa kimataifa hivyo usikubali kukaa nyumbani njoo uishuhudie Simba ya ubaya ubwela na inaongeza pumzi ya moto hii sio ya kukosa kwa kweli kwa kuna kitu kimeongezeka.

“Usifikiri kwa kuwa uliiona Simba ikicheza na Fountain Gate mchezo wake uliopita ukadhani umemaliza hapana kuna kazi kubwa inakwenda kufanyika na wachezaji wapo tayari mashabiki mjitokeze kwa wingi mpate burudani.”

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi cha Simba kwa sasa ni Kibu Dennis, Awesu Awesu, Hussen Abel, Aishi Manula.

SOMA NA HII  WAKATI RUVU WAKIOMBA MUNGU SAYIWAKUTE LEO...MBRAZILI SIMBA APANGA KUSHINDILIA NONDO...