Home Habari za Simba Leo FADLU DAVIDS AWAPA NENO MABEKI WAKE.

FADLU DAVIDS AWAPA NENO MABEKI WAKE.

HABARI ZA SIMBA-FADLU

KOCHA Mkuu wa Simba Fadlu Davids ameuzungumzia ubora wa mabeki wake wa kati, Che Malone Fondoh,  Chamou Karaboue, Hussein Kazi na haswa Abdulrazack Hamza.

Fadlu anaamini kila mmoja atakuwa na nafasi ya kupigania timu hiyo kulingana na wingi wa michezo uliopo mbele yao kuanzia katika mashindano ya ndani hadi kimataifa.

“Msimu huwa na mambo mengi, muda mwingine kuna vitu ambavyo ni ngumu kuvidhibiti mfano majeraha, ni vizuri kuwa na wachezaji wenye ubora wa namna yao ili wakati ambao mmoja anakosekana basi anakuwepo mwingine wa kuendeleza gurudumu, binafsi natamani kuwa nao wote wakiwa fiti,” alisema.

SOMA NA HII  COASTAL UNION WAINGILIA KATI USAJILI WA LAWI...SIMBA HAWAKUFUATA TARATIBU.