Home Habari za Simba Leo NANI KAMA MOHAMMED HUSSEIN…MIAKA 15 KWENYE UBORA ULE ULE

NANI KAMA MOHAMMED HUSSEIN…MIAKA 15 KWENYE UBORA ULE ULE

Habari za simba- Mohammed Hussein

Mohammed Hussein kwa sasa ndie Beki bora zaidi wa kushoto Tanzania imepata kuwa nae kwa miaka 20 iliyopita kwenye soka letu, bila shaka anaweza kuingia kwenye vitabu vya Beki bora zaidi wa kushoto kwenye historia ya mpira wetu.

Wakitaka kubishana tunakuja kwenye vigezo vya ubora ambavyo ndio daraja.

1- Consistency, wamekuja Mabeki wangapi wa kushoto pale Simba? Kitaifa na Kimataifa? Bado Mohammed akasalia kwenye ubora wa huu sana, mwendelezo wa ubora sio kitu rahisi! Nitajie beki wa kushoto kwenye level hizi.

2- Longevity, kwa maana ya muda wake ambao amehudumu kwenye soka, ni zaidi ya miaka 15 tena kwenye kiwango cha juu sana, mtaje Beki wako wa kushoto zaidi ya Mohammed Tshabalala, level hii hana historia ya majeraha ya muda mrefu kutokana na mtindo wake wa maisha.

3- Mafanikio, akiwa na kitambaa ama bila kitambaa Mohammed Hussein anaingia kwenye orodha ya Manahodha waliotwaa vikombe vingi na kucheza michuano mikubwa kwa klabu na taifa kwa mafanikio, nitajie Beki wako wa kushoto kwenye kariba hii.

4- Nidhamu, iwe ndani ama nje ya uwanja bila shaka ni sifa nyingine unapotaja neno ubora, sikumbuki naomba mnikumbushe huenda nimesahau, Tshaba ana red card? Kama zipo sidhani kama zinazidi tatu, moja kati ya Wachezaji wenye nidhamu kubwa mno.

Beki bora zaidi wa Kushoto kwenye historia ya nchi yetu.

SOMA NA HII  HUYU GUEDE ANA BALAA...NONGA ASIMULIA