Home Habari za michezo ASALALEKI… GAMONDI NA FADLU PRESHA YA DABI YAWAINGIA.

ASALALEKI… GAMONDI NA FADLU PRESHA YA DABI YAWAINGIA.

HABARI ZA SIMBA NA YANGA

KARIAKOO DABI Imeanza kunoga, zikiwa zimesalia siku chache tu kupigwa kwa mchezo unaovuta hisia kali za mashabiki wa soka nchi na Afrika na duniani kwa ujumla, Simba na Yanga.

Joto kali limehamia kwa makocha wa timu hizo mbili, Fadlu Davids kwa upande wa Simba na Miguel Gamondi kwa Yanga.

Fadlu Davids, amesisitiza nidhamu ya kiufundi na kiakili, akisema:

“Tunajua ubora wa Yanga, lakini tunajiandaa kimkakati. Lazima tuwe makini kwa kila dakika, kujenga mashambulizi kwa kasi na kudhibiti safu ya ulinzi kwa umakini mkubwa.”

Fadlu anaamini kutumia fursa chache zinazopatikana ni muhimu, akiongeza kwa kusema: “Katika mechi kama hizi, nafasi ni chache, hivyo tunahitaji kuwa bora katika kumalizia.”

Kwa upande wa Miguel Gamondi ambaye amekuwa ni tishio kwa Simba baada ya kuwapiga bao 5 na kuwafunga tena nyingine 2 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili, yeye anasema kwamba;

“Simba ni timu kubwa yenye wachezaji wenye vipaji vikubwa na historia ya mafanikio. Tunawaheshimu sana kama wapinzani, lakini tunajipanga vizuri kwa mchezo huu.

“Tunafahamu wanavyocheza na nguvu yao, lakini tutatumia maandalizi yetu kuleta ushindani na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwa kutumia nafasi kufunga mabao.” Kocha Gamondi.

SOMA NA HII  STRAIKA SIMBA AFUNGUKA ALIVYONYIMWA NAULI MOROCCO...AFICHUA MICHEZO MYAO MICHAFU...