Home Habari za Simba Leo PAUL MKAI ACHAGUA KUANZA NA CHASAMBI MBELE YA MUTALE.

PAUL MKAI ACHAGUA KUANZA NA CHASAMBI MBELE YA MUTALE.

Mtangazaji na mwandishi wa habari za michezo nchini, Paul Mkai amesema kwamba ukiwaweka wachezaji wawili wa Simba Joshua Mutale na Ladack Juma Chasambi, basi yeye ataanza na Chasambi kwa sababu zifuatazo;

“Twende na hoja ukiniuliza Paul Mkai kati ya

CHASAMBI na BUDO MUTALE unakwenda na nani?

Hakika kabisa Jibu lisilo na shaka yoyote nakwenda na LADACK CHASAMBI.

Kwa nini CHASAMBI?… Kwanza kasi yake na maarifa ni miongoni mwa mambo ambayo yanambeba kiasi cha kumfanya kuwa na madhara kwa mpinzani.

Pili ni mchezaji ambaye anajua muda sahihi wa kuachia/ kukaa na Mpira, inapobidi kuachia Mali anafanya hivyo kwa wakati na mara nyingi pasi zake zimekuwa na macho.

Kuhusu MUTALE sio mchezaji mbaya japo mambo bado hayajakaa sawa mpaka sasa ndani ya Simba SC.

Wakati Simba SC inamsajili Joshua Mutale kutoka Power Dynamos ya Zambia aliitumikia klabu hiyo ya Zambia kwenye michezo (26) amefunga Mabao (5) na kutoa pasi za mabao (3).

Mutale ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani (Versatile player), anaweza kutumika Kama Winga wa Kulia/kushoto au hata kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Shida ambayo ninaiona kwa Budo Mutale hadi sasa ni kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati, mara nyingi Miguu yake imekuwa na kigugumizi kwelikweli pamoja zao lake la mwisho ni haba.

Hivyo basi Mimi Paul Mkai “MKALI WA DIMBA” naenda na LADACK CHASAMBI mbele ya JOSHUA MUTALE “SGR”.

SOMA NA HII  KIBU DENIS MGENI RASMI SIMBA vs YANGA....KIINGILIO CHA 'MATAJIRI' CHATANGAZWA...