BAADA ya Februari 24 2025 ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 2-2 Azam FC mabosi hao wakigawana pointi mojamoja na matajiri wa Dar, Azam FC, Simba wametoa tamko lao kuhusu aina ya matokeo hayo.
Kupitia kwenye ukurasa wa Instagram wa Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameandika namna hii: Sare dhidi ya Azam FC isitufanye tujitoe kwenye mbio za ubingwa sisi wenyewe.
Pamoja na kwamba matokeo yametuumiza lakini yasiwe ni matokeo ya kutukatisha tamaa kwenye kupigania malengo yetu ya msimu.
“Tumepata sare dhidi ya timu bora na mshindani wa kweli hivyo hatuna sababu ya kukaa kinyonge. Tusiiinamishe vichwa chini mapambano yaendelee tena kwa kujiamini kwani nafasi ya mafanikio ni kubwa sana kwetu
“Ubaya Ubwela hauna side Mirror hivyo hatuna budi kuangalia nyuma tunapaswa kusonga mbele kwa mwendo wa ngiri. Tuna michezo 10 imesalia hii ni kufa na kupona, tunapaswa kushinda michezo yote na hilo tunaliweza,
“Mafanikio yetu msimu huu yapo kwenye mechi hizi 10. Nichukue nafasi hii kuwaomba Wana Simba, tuachane na kilichopotea tujikite kwenye kutafuta kilicho mbele yetu.”
SOMA NA HII MARUFUKU MPYA YA MORRISON KUKANYAGA SAUZI NI NOMA...BARBARA ASEMA TAARIFA SI ZA KWELI...