Taifa Stars–Morocco Yafutwa, Majeruhi Watano Wavuruga Mpango Wa Gamondi
Taifa Stars haitacheza tena mchezo wa kirafiki dhidi ya Morocco uliokuwa umepangwa Oktoba 5 mjini Tangier, baada ya ripoti ya madaktari kambini kuonyesha wachezaji watano wamepata majeraha yanayowafanya washindwe kuwa tayari kwa mchezo huo.
TFF imesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kushauriana na Kocha Mkuu Miguel Gamondi. Stars ilikuwa imesafiri na wachezaji 23 kwa mchezo wa kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Madagascar kabla ya kuendelea na ratiba ya kirafiki nchini Morocco.
Majeruhi Watano Wabadilisha Ratiba
Kufutwa kwa mchezo huo kunakuja wakati Stars ikiwa imetoka kwenye siku ngumu Morocco. Baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Madagascar, kikosi hicho kilipokea kipigo cha mabao 5-0 kutoka AS FAR Rabat katika mchezo wa kirafiki, matokeo yaliyoongeza maswali kuhusu ulinzi na namna timu inavyoanza mechi.
Sasa Gamondi hatapata tena nafasi ya kuitumia Morocco kama kipimo kingine cha moja kwa moja. TFF haijataja majina ya wachezaji watano waliojeruhiwa wala aina ya majeraha yao, huku pia ikiwa bado haijaweka wazi kama kutakuwa na mchezo mwingine wa kuchukua nafasi ya Morocco.
Gamondi Anakosa Kipimo Kikubwa
Kwa benchi la ufundi, hii ni setback kwa sababu Morocco ilikuwa mechi ambayo ingeweza kumpa Gamondi picha nyingine kuhusu uwezo wa kikosi chake mbele ya timu yenye ubora mkubwa. Baada ya mabao matano ya AS FAR, kocha angehitaji kuona reaction ya wachezaji wake, hasa kwenye concentration, organisation ya mabeki na namna ya kuzuia mashambulizi ya haraka.
Kwa upande mwingine, afya ya wachezaji ndiyo imepewa kipaumbele. Kama tayari kuna kundi la wachezaji watano ambao hali zao haziruhusu kucheza, kuendelea na friendly nyingine yenye intensity kubwa kungeweza kuongeza tatizo kabla ya wachezaji kurejea katika klabu zao.
Safari Ya Morocco Imeacha Maswali
Stars inaondoka kwenye dirisha hili ikiwa na pointi moja dhidi ya Madagascar, kipigo kizito dhidi ya AS FAR na sasa mchezo wa Morocco umefutwa. Hivyo kazi kubwa ya Gamondi itakuwa kuchukua kila kilichotokea na kukigeuza kuwa somo kabla ya ratiba inayofuata.
Soma Hapa: Taifa Stars Yapigwa 5-0 Na AS FAR, Gamondi Apata Tahadhari Nzito Morocco