STARS YAPIGWA 3-0 NA ALGERIA AFCON, SASA KUPANDA NDEGE TAYARI KUREJEA NYUMBANI
Kikosi cha Taifa Stars kimekamilisha rasmi safari ya michuano ya AFCON huko Misri kwa kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Algeria.Katika mchezo huo wa kundi C, Stars imepokea kichapo cha tatu mfululizo baada ya kufungwa na Senegal kwa mabao 2-0 kisha Kenya kwa mabao 3-2.Mabao ya Algeria usiku huu yamewekwa na Islam Silmani pamoja na Adam Ounas aliyeingia...
KMC WAIWAHI MAPEMA TP MAZEMBE
KIKOSI cha timu ya KMC Alhamisi hii kinatarajia kukwea pipa kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya kuwawahi wapinzani wao TP Mazembe katika michuano ya Kombe la Kagame.KMC ambao wanafundishwa na kocha Jackson Mayanja raia wa Uganda, ni miongoni mwa timu shiriki za kombe hilo la Kagame ambapo walipata nafasi hiyo baada ya Yanga na Simba kujitoa.KMC wamepangwa Kundi B...
KOCHA MBRAZIL APONGEZA SILVER NA FRAGA KUSAJILIWA SIMBA ‘ WAMEPATA VIFAA’
KOCHA Mbrazil aliyewahi kutamba na Taifa Stars na Azam, Itamir Amorin ameukubali usajili wa Wabrazil uliofanywa na Simba inayojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza Agosti 9.Itamir ambaye aliletwa Tanzania na Kocha Mbrazil mwenye heshima, Marcio Maximo kama msaidizi wake na mtaalam wa viungo wa Taifa Stars, ameliambia Spoti Xtra kwa njia ya simu kutoka Rio De Janeiro nchini...
MARCUS RASHFORD NI POCHI NENE MANCHESTER UNITED BAADA YA KUSAINI MKATABA MPYA
MARCUS Rashford ameingia makubaliano na timu yake ya Manchester United kwa kandarasi ya miaka minne huku akilipwa mshahara mnene.Rashford ambaye ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya England kwa sasa atakuwa analipwa Pauni 300,000 kwa wiki kwa mujibu wa mkataba wake mpya.Mkataba huo utamalizika mwaka 2023, Rashford atalipwa jumla ya Pauni 200,000 kwa wiki akiwa ndani ya Old Trafford...
NIYONZIMA WA SIMBA KUIBUKIA CONGO
Imeelezwa kuwa kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na timu ya As Vita ya Congo.Niyonzima ametangaza kuachana na Simba baada ya mkataba wake kumalizika hivyo kwa sasa yupo huru kujiunga na timu atakayokubaliana nayo.Niyonzima amesema kuwa wakati wake ukifika wa kutaja timu atakayotua msimu mpya atawaambia mashabiki.
BEKI MPYA YANGA ATUMA UJUMBE MZITO KWA WAPINZANI
BEKI mpya wa Yanga ambaye kwa sasa yupo na timu ya Taifa nchini Misri, Ally Mtoni 'Sonso' amesema kuwa ana imani ya kufanya makubwa msimu ujao ndani ya kikosi chake kipya.Sonso amesema kuwa kwa namna anavyomtambua beki mkongwe Kelvin Yondani itakuwa ngumu kwa wapinzani kupita ukuta wa Yanga."Natambua uwezo wa Yondani ndani ya Yanga, hivyo uwepo wangu ndani ya...
VIGOGO 10 WATEULIWA NDANI YA YANGA KAMATI YA FEDHA
MWENYEKITI wa Yanga, Dr. Mshindo Msolla kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji amewateua wajumbe 10 kuunda Kamati mpya ya Fedha na Mipango.Orodha ya walioteuliwa ndani ya Yanga kwenye Kamati hiyo hii hapa:-Arafat Haji nafasi ya Mwenyekiti.Shija Richard nafasi ya Makamu Mwenyekiti.Deo Mutta yeye ni Katibu.Kwa upande wa wajumbe ni pamoja na :- Said Kambi, Ally Mayay, Pindu Luhoyo, Baraka...
WAWA APIGWA PINI SIMBA
PATRICK Wawa, beki kisiki wa Simba ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu yake.Wawa alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotwaa kombe la Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 hivyo anarejea kuendelea kuongoza kazi ya ulinzi ili kutetea taji tena msimu ujao.
STARS KUFANYA MAAJABU LEO AFCON
MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa ya Tanzania, 'Taifa Stars' Simon Msuva amesema kuwa leo watapambana kufanya vema kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Algeria.Stars haijawa na matokeo chanya kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri baada ya kupoteza michezo yote miwili waliyocheza hatua ya makundi na leo watamenyana na Algeria."Tulipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal, tuliumia, tukapoteza pia...
SIMBA YAINGIA MKATABA NA KAMPUNI YA A-ONE, YAVUNA MAMILIONI
KLABU ya Simba,imeingia mkataba na Kampuni ya A-one kwa ajili ya kutangaza bidhaa yao mpya ya Mo xtra Energy wenye thamani ya Tsh.Milioni 250.Mkataba huo umesainiwa leo na Meneja Masoko wa A-One, Fatma Dewji na Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori ambapo umesainiwa ukiwa mwendelezo wa mkataba wa timu hiyo na kampuni hiyo.Hii ni mara ya Pili kwa Simba...