MTAMBO MPYA YANGA WATUA UWANJA WA NDEGE DAR
Mshambuliaji wa kimataifa wa Namibia Sadney Urikhob amewasili tayari Tanzania kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Yanga.Urikhob ametua nchini na sasa ataelekea mjini Morogoro kujiunga na wenzake kwa ajili ya kambi maalum inayoendelea.Mshambuliaji huyo alishamalizana na Yanga kwa kuingia nao mkataba wa miaka miwili.Pro huyo amepokelewa na viongozi wa Yanga katika Uwanja wa Ndege na sasa kinachofuata ni...
EXCLUSIVE!! MZEE KILOMONI SI MDHAMINI TENA SIMBA SC, USHAHIDI HUU HAPA
Hizi ni barua zilizotoka kwa kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali kwenda kwa wakili wa aliyekuwa mdhamini wetu, na pia barua ya Mahakama kwenda kwa wakili huyo zinazothibitisha mdhamini huyo Mzee Hamis Kilomoni siyo mdhamini tena wa klabu yetu ya Simba.Taarifa hii ilitolewa leo na Afisa Mtendaji Mkuu, Crescentius Magori kwenye mkutano wake na wanahabari.
CHALII WA ARUSHA ALIVYOBEBA MPUNGA WA SPORTPESA
Mkazi wa Arusha Bwana Revocatus M. Majura akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi 10,317,378 baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 11 kati ya 13 kwenye Jackpot ya SportPesa. Kulia ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano SportPesa, Bi Sabrina Msuya.
HILO DAU LA LEROY SANE WA MANCHESTER CITY LAZIMA UKAE
UONGOZI wa timu ya Bayern Munich umethibitisha suala la kuitaka saini ya winga wa Manchester City, Leroy Sane.Mwenyekiti wa klabu hiyo, Kari Heinz Rummenigge amekiri kuwa klabu yake inaiwinda saini ya nyota huyo wa Manchester City.Rumminigge amesema kuwa hata hivyo klabu hiyo inahitaji mkwanja mrefu ili kuwapa nyota huyo.City wanahitaji dau la shilingi pauni milioni 100 ili kumuachia nyota...
CAF YAIRUHUSU SIMBA KUTINGA JEZI YA KIJIVU
UONGOZI wa Simba umesema kuwa msimu ujao Simba watatumia jezi ya rangi nyekundu nyumbani na rangi nyeupe ugenini huku wakitumia rangi ya kijivu pale timu zinapogongana rangi.Mtendaji mkuu wa timu ya Simba, Crecentius Magori amesema kuwa mpango huo ni kutokana na utaratibu wa Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) "Timu imeweka kambi nchini Afrika Kusini ikiwa ni maalumu kwa ajili...
DIDA; NINA OFA TANO MKONONI KWA SASA
Deogratius Munish, mlinda mlango huru baada ya kuachana na Simba amesema kuwa ana ofa tano mkononi mwake kwa sasa.Dida hana timu na anatumia muda mwingi kujifua ili abaki kwenye ubora wake anatajwa kujiunga na timu ya Mtibwa Sugar ambayo amewahi kuitumikia.Dida amesema kuwa kwa sasa bado mazungumzo yanaendelea na taratibu zikikamilika atataja timu atakayokwenda."Nina ofa tano mkononi kwa timu...
YONDANI AAHIDI MACHUNGU KWA WAPINZANI
BEKI mwenye nafasi kubwa ya kupewa unahodha wa Yanga msimu ujao, Kelvin Yondani amekiri kwamba kikosi hicho kimesheheni.Mchezaji huyo wa zamani wa Simba, alisema ana uhakika kwamba timu hiyo itacheza soka la kueleweka sasa kutokana na kusajili mafundi wanaojua. Lakini amekiri kwamba kwenye nafasi yake kuna ushindani mkubwa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa lakini hajawahi kufeli wala kuhofia...
AJIBU AWATAKA SIMBA WATULIZE BOLI, MSIMU NI WAO
Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu.Ajibu ambaye msimu uliopita wa 2018-19 alikuwa kinara wa asisti ndani ya ligi akiwa nazo 17 na pia alitupia mabao sita kwa sasa ni mali ya Simba ambapo amesaini kandarasi yamiaka miwili.“Bado msimu haujaanza, utakuwa muda mzuri kwetu kujipanga vema kwa ajili...
MWADUI FC WASHINDA VITA YA KUIPATA SAINI YA NYOTA WA MTIBWA SUGAR
Mwadui FC imeshinda vita ya kuipata saini ya beki wa Mtibwa Sugar, Rojas Gabriel ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.Gabriel alikuwa anawindwa na timu ya Kagera Sugar , Singida United na Namungo ambapo Mwadui FC waliikomalia saini yake mpaka akakubali kumwaga wino.Akizungumza na Saleh Jembe, Gabriel amesema kuwa anafurahi kupata changamoto mpya atapambana kutimiza majuku yake."Kazi yangu ni mpira...
HUYU NDIYE PILATO WA FAINALI YA AFCON KATI YA SENEGAL NA ALGERIA
BAMLAK Tessema mwenye umri wa miaka 39 raia wa Ethiopia ameteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuchezesha mchezo wa fainali ya michuano ya Afcon utakaochezwa Ijumaa kati ya Senegal na Algeria uwanja wa kimataifa wa Cairo.Fainali inatajwa kuwa na msimko wa kipekee kutokana na timu zote mbili kuhitaji kuwa mabingwa wa michuano hii mikubwa.Algeria na Senegal wote walikuwa...