DU SANCHEZ NOMA ANAKUNJA MKWANJA MREFU BALAA, UWANJANI NAKO BALAA
ALEXIS Sanchez staa wa Chile anayekipiga Manchester United anashika namba moja kwa kulipwa mkwanja mrefu ndani ya Ligi Kuu England.Mshahara wake kwa mwezi anaolipwa na mabosi zake United ni pauni milioni mbili sawa na sh. bilioni 5.7.Licha ya kukunja mkwanja huo mrefu uwanjani amepachika mabao matano tu na amecheza mara 45 tangu alipojiunga na kikosi hicho akitokea Arsenal.
UNITED YAPATA KIGUGUMIZI KUZUNGUMZIA ISHU YA LUKAKU, YAIKOMOA MILAN
INTER Milan sasa wanatakiwa kulipa dau la pauni milioni 90 ili kumpata mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku.Raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26 anahusishwa kujiunga Milan na kukikacha kikosi cha United kilicho chini ya meneja ole gunnar solskjær ambaye amesema kuwa hawezi kuweka wazi kama anahitaji kubaki naye ama la."Kile ambacho huwa naongea na wachezaji wangu...
NEYMAR JR MKOROFI, KICHAPO CHA MABAO 6-1 WALICHOKIPATA PSG ADAI HAJAKISAHAU
NEYMAR Jr mwenye miaka 27 bado ameendelea kushinikiza ndani ya klabu yake ya PSG apewe ruhusa ya kusepa mazima.PSG bado hawajakubali kumuachia nyota huyo ndani ya kikosi hicho kutokana na uhitaji waloonao ilihali mwenyewe hana furaha ya kubaki ndani ya kikosi chicho.Neymar amesisitiza kuwa kumbukumbu yake njema kwenye soka ni kitendo cha Barcelona kuinyoosha PSG mabao 6-1 kwenye Ligi...
SENEGAL WAMESOTA KWELI BILA KUTINGA HATUA YA FAINALI AFCON
TIMU ya Senegal haijawahi kutwaa kombe la Afcon na Ijumaa watakuwa na kibarua cha kumenyana na Algeria kwenye mchezo wa fainali.Mara ya mwisho Senegal kutinga hatua ya fainali ilikuwa ni mwaka 2002 na muda huo kocha wao Alliou Sisse maarufu kwa jina la Rasta alikuwa akicheza nafasi ya kiungo mkabaji.Imepita miaka 17 tangu watinge hatua hiyo ya fainali ya...
YANGA YALETA BEKI SPESHO
UONGOZI wa Yanga umekamilisha taratibu za usajili wa beki wa kushoto wa Rayon Sports ya Rwanda, Ericky Rutanga anayejiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo Ligi Kuu Bara maalum kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Awali, Yanga iliwahi kumfuata beki huyo na kuzungumza naye na kushindwa kufikia muafaka mzuri na kusalia Rayon huku Gadiel Michael aliyekuwa akicheza...
MO ALIAMSHA TENA HUKO
MWEKEZAJI wa Simba, Mohamed Dewj, leo ameandika ujumbe mfupi ambao umeacha maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa soka kutaka kujua maana ya maneno hayo.Mo amekuwa na kawaida ya kuandika ujumbe mfupi kwenye kurasa zake ambao umekuwa ukiacha maswali mengi kwa wanaomfuatilia kwa sasa.Kupita ukurasa wake wa Instagram, Mo ameandika namna hii : "Uongo unapanda kwa lifti.Ukweli unapanda kwa...