STRAIKA SIMBA ASAINI AFRIKA KUSINI
MSHAMBULIAJI wa Simba, Adam Salamba ametua rasmi katika kikosi cha TS Sporting ya Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa mkopo wa mwaka mmoja.Salamba alisajiliwa na Simba msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Lipuli FC ya Iringa kwa dau la Sh mil 30 na gari.Awali iliripotiwa kuwa, Salamba angejiunga na Klabu ya Polokwane City ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Afrika...
OKWI AGOMEA MKATABA SIMBA
EMMANUEL Okwi amezidi kuwatia kiwewe Simba kwanza kutokana na kiwango anachokionyesha kwenye michuano ya Kombe la Afrika ‘Afcon’ kule Misri pili ni kuwa anazingua kusaini mkataba wa miaka miwili Msimbazi.Okwi, raia wa Uganda, amefanikiwa kuibuka mchezaji bora wa mechi kwenye Afcon katika mchezo wa kwanza dhidi ya DR Congo ambapo yeye alifunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0...
MTUPIAJI MWINGINE TENA ANASWA KMC
VITALIS Mayanga leo amejiunga na KMC kwa kandarasi ya mwaka mmoja akitokea klabu ya Ndanda. Mayanga akiwa ndani ya Ndanda msimu wa 2018/19 alitupia jumla ya mabao 10 anaungana na Salim Aiyee ambaye msimu uliopita alitupia mabao 18, amesaini kandarasi ya miaka miwili.Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanga amesema kuwa ni muda wake kupata changamoto mpya shemu nyingine.
SINGIDA UNITED YASAJILI MAJEMBE MAWILI
KLABU ya Singida United leo imeanza rasmi usajili wake kuelekea msimu ujao kwa kuwasajili majembe mawili. Beki wa kushoto, Salum Marcelo ambaye alikuwa akitumikia Malindi FC na mshambuliaji, Herman Frimpong kutoka Ghana wamesaini kandarasi ya miaka mitatu.Ofisa Habari wa Singida United Cales Katemana amesema kuwa wataanza kambi rasmi Julai Mosi mwaka huu.
DIRISHA LA USAJILI BARA LAFUNGULIWA KWA CAF NA LIGI KUU, FAINI ZATAJWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kufunguliwa kwa Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2019/2020.Dirisha litafungwa Julai 31, 2019 na hakutakua na muda wa ziada.Usajili wa mashindano ya CAF kwa klabu za Simba,Young Africans, Azam FC na KMC wenyewe utafungwa Julai 10, 2019.Baada...
MANCHESTER UNITED WATAJA DAU LA POGBA
MANCHESTER United wamekubali kwa sasa mambo yaishe kwa kiungo ,Paul Pogba ambaye ameomba kusepa ndani ya kikosi hicho.United wamenyoosha mikono baada ya kuamua kutangaza dau la kumuuza mchezaji huyo ambaye anatajwa kujiunga na Real Madrid ama Juventus.United imesema kuwa dau la mchezaji huyo kwa timu inayotaka huduma yake inapaswa iangushe mezani kiasi cha pauni milioni 150 kupata saini yake.
HATMA YA AJIBU KUTUA SIMBA KUJULIKANA LEO
MENEJA wa Ibrahimu Ajibu, Athuman Ajibu amesema kuwa timu atakayojiunga mteja wake itajulikana.Ajibu alikuwa anatakiwa kujiunga na TP Mazembe dili hilo liliyeyuka kwa kile kilichoelezwa dau kubwa huku akitajwa tayari amemalizana na Simba.Akizungumza na Saleh Jembe, Ajibu amesema kuwa kwa sasa mambo bado ni magumu kwake hivyo mpaka jioni atakuwa amemaliza kazi.“Kwa sasa mambo bado hayajawa sawa, itafahamika leo timu...
HATMA YA AJIBU KUJIUNGA NA SIMBA HII HAPA
MENEJA wa nyota wa Yanga, Ibrahim Ajibu, Athuman Ajibu amesema kuwa kwa sasa suala la timu atakayojiunga mteja wake Ajibu bado ni pasua kichwa hivyo kesho anaamini mipango itakuwa imekamilika.Ajibu alikuwa anahitajika kujiunga na TP Mazembe aliamua kuzingua kwa kile kilichoelezwa kwamba ni dau dogo na sasa imeelezwa kuwa hana nafasi ndani ya Yanga.Akizungumza na Salehe Jembe, Ajibu amesema...
NYOTA MPYA KMC AIYEE AKIWASHA
MSHAMBULIAJI mpya wa KMC, Salim Aiyee ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili amesema kuwa msimu ujao atatacheka na nyavu mpaka achoke.Aiyee akiwa Mwadui FC alitupia jumla ya mabao 18 kwenye ligi kuu msimu wa 2018/19."Nimetua KMC kufanya kazi maalumu ambayo naipenda, msimu ujao nitafunga mengi zaidi ya niliyofunga Mwadui FC, sapoti na ushirikiano ni jambo la msingi," amesema.
NYOTA WA SIMBA AMCHIMBA MKWARA MO SALAH
NYOTA wa timu ya Taifa ya Uganda na timu ya Simba, Juuko Murshid amesema kuwa yupo fiti kumenyana na Misri bila kuhofia uwepo wa nyota Mohamed Salah anayekipiga Liverpool.Uganda itamenyana leo na Misri uwanja wa Cairo International ikiwa ni mechi ya mwisho kwenye kundi A ambalo Misri anaongoza akiwa na pointi sita huku Uganda wakiwa na pointi nne nafasi...