Tuesday, January 13, 2026
Home Blog Page 2952

MABOSI SIMBA WAACHANA NA OKWI

0


MABOSI wa Simba wameuweka pembeni mkataba wa Emmanuel Okwi kwa kile kilichotajwa kutaka dau kubwa la usajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Mganda huyo hivi karibuni aliwaaga mashabiki wa timu hiyo kwa kupitia mtandao wa kijamii kwa kuweka picha yake na ujumbe wa kuaga ambao ulizua mjadala mkubwa.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, Okwi anataka dau kubwa zaidi ya msimu uliopita la kusajiliwa ambalo ni Shilingi Milioni 115  alilosajiliwa pia Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kama mshambuliaji huyo akiendelea na kung’angania dau hilo, basi hawataendelea nae msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa na badala yake watamsajili mwingine mbadala wake mwenye uwezo zaidi yake.

“Kikosi chetu cha msimu ujao kinatarajiwa kuwa mabadiliko makubwa kwa kusajili wachezaji wenye uwezo na uzoefu wa kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika tutakayoshiriki, mwakani na kubwa zaidi kulichukua taji hilo. “Hivyo, tulichopanga ni kusajili wachezaji waliowahi kuzipa mafanikio timu zao kupitia michuano mikubwa Afrika, hivyo kwa gharama yoyote tutakuwa tayari kumsajili mchezaji kutoka nje ya nchi.

“Hivyo, huyo Okwi kama anataka kuondoka milango ipo wazi, kama uongozi haupo tayari kutoa dau hilo la usajili analolitaka kutokana na kiwango chake alichonacho hivi sasa katika kuelekea michuano mikubwa Afrika,”alisema mtoa taarifa huyo licha ya kutotaka kutaja dau lenyewe.

Alipotafutwa Mkurugenzi Mtendaji (C.E.O) wa klabu ya Simba kuzungumzia hilo alisema kuwa “Hilo suala litajulikana hivi karibuni kwani tayari uongozi umeshaanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji watakaongeza mikataba yao na kati ya hao yupo huyo Okwi tusubirie kila kitu kitajulikana.”

CHANZO: CHAMPIONI

SAMATTA AUNGANA NA SERIKALI KUFANYA JAMBO LA KIHISTORIA

0


SERIKALI imesema itaendelea kumsaidia kwa hali na mali Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, anayechezea Klabu ya Genk ya Nchini Ubelgiji Mbwana Samatta ili kuhakikisha kuwa anafungua milango ya uwekezaji na kuiweka juu ramani ya Soka la Tanzania katika anga la kimataifa.

Akizungumza jana Jumanne (Mei 28, 2019) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na Nahodha huyo waTaifa Stars, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema Samatta ameonyesha njia iliyoshindwa kufikiwa na wachezaji wengi wa miaka ya nyuma waliojaribu kucheza Soka la kulipwa katika vilabu mbalimbali vya Nchi za Nje hususani Bara la Ulaya.

Dkt. Abbasi alisema Serikali ilimteua Sammatta kuwa Balozi wake wa Utalii kutokana na sifa kubwa zilizoletwa na mchezaji huyo nje ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa Serikali ina Imani naye kubwa katika kufungua milango ya fursa za uwekezaji hususani katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano hapa nchini.

“Mbwana Samatta ameonyesha njia ambayo ilikuwa ndoto iliyoshindwa kutimizwa na wachezaji wengi wa zamani, hatua hii aliyofikia ni kubwa na imetokana na sifa kubwa ya nidhamu na kipaji cha mchezo huu hili ni funzo kwa wachezaji wetu chipukizi” alisema Dkt. Abbasi.Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alisema kwa sasa yapo mambo makubwa na mazuri hususani vivutio vya sekta ya utalii, hivyo kupitia nafasi yake ya Ubalozi Serikali itatoa msaada wowote unaohitajiwa na mchezaji huyo ili kuhakikisha kuwa vivutio vya Tanzania vinabainishwa na hivyo kutangaza mambo mazuri ya Tanzania.

Aidha Dkt. Abbasi alisema Ofisi yake imeandaa mikakati mbalimbali ya mawasiliano ya kitaifa katika kuisema nchi katika maeneo mbalimbali hivyo kumtaka mchezaji huyo kutumia majukwaa hayo kwa ajili ya kuona namna bora ya kutumia fursa hizo ili kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi alimtaka mchezaji huyo kuwasiliana naye iwapo kutakuwepo na changamoto yoyote anayoweza kuipata katika kutekeleza majukumu yake ya nafasi ya Ubalozi kwani kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano imefungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Kwa upande wake, Nahodha huyo wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alisema akiwa nchini Ubelgiji tayari amefanya juhudi kubwa katika kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini, ambapo mwanzoni mwa mwezi ujao madaktari 5 wa timu hiyo wanatarajia kuja nchini kwa ajili ya kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii nchini.

Samatta alisema raia wengi wa kigeni wana shauku ya kutembelea Tanzania kutokana kusikia na kuona uzuri wa vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Wanyama, hivyo akiwa Balozi wa Utalii afanya kila liwezekanalo kukaa karibu na viongozi na wachezaji wa klabu yake ya KRC Genk kuwaeleza uzuri wa Tanzania ili na wao waonesha nia ya kuitembelea Tanzania.

“Wachezaji wengi hususani wale wa kiafrika waliopo nje hususani Bara la Ulaya wanaipenda sana Tanzania, na hi inatokana na sifa tuliyonayo, na hivyo kwa kutumia nafasi yangu ya Ubalozi nitaendelea kushawishi waitembelee Tanzania” alisema Samatta.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Samatta Tours, Hamis Waziri aliishukuru Serikali kutokana na jitihada mbalimbali inazofanya kwa ajili ya kuhamasisha sekta ya utalii nchini na kusema taasisi hiyo itakuwa tayari kutangaza matukio mbalimbali kwa ajili ya kulitangaza jina la Tanzania.

BREAKING NEWS: BODI YA LIGI YAKIRI KUBORONGA, YAISHUSHA STAND UNITED, KAGERA YAENDA PLAY OFF

0


Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imetangaza kufanya marekebisho katika msimamo wa Ligi Kuu Bara huku ikisema itachukua hatua kwa watunza takwimu wake waliopotosha.

Awali ilionekana Kagera Sugar ndio imeteremka lakini Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema marekebisho waliyofanya Stand United inashuka na nafasi ya juu inakwenda kwa Kagera Sugar.

Maaana yake Stand United ndio iliyoteremka daraja na nafasi ya kucheza Play Off inakwenda kwa Kagera Sugar.

Kagera Sugar itaivaa Pamba Juni 2 katika mechi ya Play Off na mshindi atacheza Ligi Kuu Bara na Mwadui FC itamenyana na Geita.

Baada ya ligi kumalizika jana, kumekuwa na gumzo na kizumgumkuti huku watu wakiwa hawajui timu iliyoteremka kwa kuwa tawimu za Gazeti la Championi na Azam Tv zilionyesha aliyeshuka ni Stand United huku takwimu za bodi ya ligi zilionyesha ni Kagera Sugar ndio iliyoteremka.

Ni Stand United, sio Kagera Sugar

0

Timu ambayo ilikuwa inasubiriwa kushuka daraja kuungana na African Lyon imepatikana rasmi. Baada ya sintofahamu kutokea jana wakati ligi ilipomalizka. Stand United ya Shinyanga  wameshuka daraja baada ya kufungwa na JKT Tanzania kwa goli 2-0 na JKT Tanzania, na kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Ligi, na si Kagera Sugar tena.

 

Timu mbili ambazo zitacheza playoff (Michezo ya mitoano ) ni Kagera Sugar aliyeshika nafasi ya 18 na Mwadui FC aliyeshika nafasi ya 17.

Mwadui na Kagera watacheza na Pamba FC ya Mwanza na Geita Sports ya Geita. Mshindi wa playoff atapanda ligi kuu Tanzania bara msimu ujao tena

The post Ni Stand United, sio Kagera Sugar appeared first on Kandanda.

NEYMAR KUUNGANA NA MESSI PAMOJA NA SUAREZ BARCELONA: TETESI ZA LEO JUMATANO HIZI HAPA

0


Mshambuliaji wa Manchester United Mbelgiji Romelo Lukaku upo tayari kukatwa mshahara ili ahamie klabu ya Inter Milan hivi karibuni. (Gazzetta dello Sport)

Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer ameipa klabu yake muda mpaka mwakani kuuza wachezaji wote asiowataka ikiwa kama sehemu ya miango yake ya kuijenga upya klabu hiyo. (MEN)
Barcelona wameamua kuendelea na kocha Ernesto Valverde kwa msimu ujao japo kulikuwa na ripoti kuwa kocha huyo alikuwa afutwe kazi. (Marca)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez amesema ana matumaini ya kumsajili Eden Hazard katika majira haya ya joto. (Onda Cero, via Mirror)

Atletico Madrid wamemchagua mshambuliaji wa Paris St-Germain na timu ya taifa ya Uruguay Edinson Cavani kama mbadala wa mshambuliaji wao Diego Costa, 30. (Cadena Ser – in French)
Newcastle United wamefanya mawasiliano na klabu ya Benfica wakiwa na nia ya kumsajili kipa wao ambaye ni raia wa Ugiriki Odysseas Vlachodimos na inaaminika Benfica wanataka kitita cha pauni milioni 13. (O Jogo – in Portuguese)

Barcelona pia inasemekana wapo tayari kumtoa kiungo Philippe Coutinho ama mshambuliaji Ousmane Dembele kwenda Paris St-Germain kama sehemu ya makubaliano ya kumpata mshambuliaji Neymar. (Record)

Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte amesaini mkataba mpya wa kuinoa klabu ya Inter Milan mpaka mwaka 2022. (Tuttomercatoweb – in Italian)

Straika wa Eintracht Frankfurt Luka Jovic yaonekana hana nia ya kuendelea kusakata kabumbu kwenye klabu hiyo baada ya kuhamisha viurago vyake kwenye kabati lake la timu kabla ya michuano ya Ulaya ya wachezaji wa chini ya miaka 21. (Bild – subscription)

Kocha wa Arsenal Unai Emery anataka kumsajili beki wa pembeni wa Ubelgiji Thomas Meunier kutoka katika klabu ya Paris St-Germain. (France Football)

HAWA HAPA WACHEZAJI PASUA KICHWA KWA ZAHERA WA YANGA

0


Ibrahim Ajibu

Kesho, Mei 30 mkataba wake unamalizika ndani ya Yanga, bado amekuwa pasua kichwa kwa kocha Mwinyi Zahera kutokana na kuvuruga dili lake la kusepa kwenda TP Mazembe na mpaka sasa hajaonana na kocha wake huyo ambaye ndiye alimshauri ajiunge na Mazembe.

Amissi Tambwe

Amekuwa bora mwishoni licha ya kuanza kwa kusuasua majeruhi yamemfanya asiwe bora, mkataba wake nae upo ukingoni kwa sasa ni mchezaji huru na bado haijawekwa bayana kama ataongezewa mkataba mpya na Yanga.

Thaban Kamusoko

Umri pamoja na kushuka kwa uwezo kwa muda kunamfanya Zahera apate kigugumizi kumuweka kwenye orodha ya wachezaji wake wapya ambao atawatumia mwaka ujao kwenye ligi.

Haruna Moshi

Timu yake ya zamani African Lyon imekwenda moja kwa moja daraja la kwanza na mkataba wake unakamilika mwishoni mwa mwezi huu hivyo atakuwa huru kwa sasa.

Mrisho Ngassa

Msimu huu amekuwa kwenye kikosi cha Yanga ambapo alitokea Ndanda FC,Zahera anamtazama kwa nafasi yake huku akipasua kichwa kujua hatma yake.

Ramadhan Kabwili

Mlinda mlango namba moja wa Yanga amekuwa bora msimu huu licha ya kutopewa nafasi mara kwa mara, kesho mkataba wake unakamilika bado hajazungumza na uongozi wa Yanga juu ya hatma yake, mbivu na mbichi zitajulikana kwani anafuatiliwa na timu moja iliyopo Sudan.

SHANGWE ZA SIMBA KUANZIA KIBAHA LEO

0

BAADA ya kutwaa ubingwa jana, mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba leo wanarejea makao makuu ya klabu Msimbazi kuendeleza sherehe za ubingwa.

Sherehe za ubingwa zitaanzia maeneo ya Kibaha, mkoani Pwani majira ya saa 5:30 ambapo wachezaji pamoja na kombe watapanda gari la wazi kuwaonyesha kombe mashabiki wao.

Mchezo wao wa mwisho jana walikubali suluhu mbele ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

329,001FansLike
12,344FollowersFollow
16,900SubscribersSubscribe

EDITOR PICKS