Home Uncategorized BEKI SIMBA ASAINI YANGA

BEKI SIMBA ASAINI YANGA


Uongozi wa klabu ya Yanga umemalizana na beki Lamine Moro kwa kusaini mkataba wa miaka miwili.

Moro ambaye ni raia wa Ghana, ambaye aliwahi kuja Simba kufanyiwa majaribio kipindi cha michuano ya SportPesa CUP, amefikia mwafaka kwa kusajiliwa na Yanga.


Beki huyo sasa atakuwa Jangwani mpaka mwaka 2021 akiihudumia timu hiyo ambayo ni bingwa wa kihistoria katika Ligi Kuu Bara.

Usajili huo unafanyika ikiwa ni jithada za Yanga kuongeza nguvu ndani ya kikosi chao tayari kwa maandalizi ya kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

SOMA NA HII  YANGA YATUMIA MILIONI KUBORESHA HOSPITALI YA MWANANYAMALA