Home Uncategorized KIBA ATAJA SABABU YA NIFUATE PROJECT, JUNI 2 KUWAKA TAIFA

KIBA ATAJA SABABU YA NIFUATE PROJECT, JUNI 2 KUWAKA TAIFA



MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba amesema kuwa sababu kubwa za kuandaa mchezo maalumu utakaochezwa jumapili uwanja wa Taifa ni kuisaidia jamii inayowazunguka.


Alikiba na Mbwana Samatta wameandaa mchezo maalumu wakiwa na kampeni yao inayokwenda kwa jina la nifuate na muunganiko wao unaitwa SAMAKIBA Foundation, unawajumuisha wanamichezo na wasanii pamoja na mashabiki wote.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ali Kiba alisema kuwa ni wajibu wao kurejesha shukrani kwa jamii inayowazunguka.

“Tumefanya hivi kwa ajili ya kusaidia na kuikumbuka jamii inayotuzunguka ambayo inakuwa na mahitaji fulani wakati fulani, sisi ni watu tunaokubalika katika jamii hivyo hatuoni vibaya kurejesha kile tunachokipata kwenye jamii,” amesema Kiba.
SOMA NA HII  MFEREJI HUU NDIO CHANZO CHA KUPIGWA CHINI ZLATKO, UNAPASWA UZIBWE