Home Uncategorized YANGA WATOA TAMKO JINGINE JUU YA NDEMLA NA MKUDE

YANGA WATOA TAMKO JINGINE JUU YA NDEMLA NA MKUDE


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ametamka kuwa hana mpango na viungo wa Simba, Jonas mkude na Said Ndemla ingawa baadhi ya viongozi wanawatamani.

Kauli hiyo ameitoa juzi kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye hoteli ya kisasa ya The Atriums Hotel iliyopo Sinza Afrikanasana jijini Dar es Salaam mara alipokutana na Waandishi wa Gazeti hili.

Zahera alisema kuwa, kwa hapa nchini timu alizopanga kwenda kufuata wachezaji kwa ajili ya kuwasajili ni KMC ya jijini Dar es Salaam na Lipuli FC na siyo Simba.

“Katika usajili wangu mpya nimepanga kusajili wachezaji tisa pekee kati ya hao wapo sita kutoka nje ya nchi na watatu wazawa badala ya wawili nilioahidi kuwasajili hivi karibuni.

“Katika usajili wangu hautakuwa na mchezaji yeyote wa Simba akiwemo huyo Mkude na Ndemla anayetajwa kuja kuichezea Yanga katika msimu ujao wa ligi. Labda nikuweke wazi kuwa sitasajili mchezaji yeyote kutoka Simba,”alisema Zahera.

SOMA NA HII  YANGA YAMTAJA ALIYEKABIDHIWA MIKOBA YA ZLATKO