Home Uncategorized BARUA YACHELEWESHA DILI LA MGHANA SIMBA

BARUA YACHELEWESHA DILI LA MGHANA SIMBA


WAKATI mkataba wa nyota wa Simba, Nicholas Gyan raia wa Ghana ukikoma mwezi ujao, imethibitika kuwa beki huyo anasubiri barua tu ili aweke wazi timu anayokwenda.

Meneja wa nyota huyo, Juma Ndambi alisema kinachowakwamisha kwa sasa ni barua kutoka Simba na wamekuwa kimya bila kueleza lolote kuhusiana na mkataba wa mchezaji huyo.

Meneja huyo aliongeza kuwa mpaka sasa wamepokea ofa kutoka klabu mbalimbali na wana- tarajia kusaini mkataba wa awali huku wakiendelea kuisikilizia Simba.

“Simba wapo kimya hawasemi lolote kuhusu mchezaji wangu na kwa sasa tunafuatilia barua tu ambayo tukipata tutaendelea na taratibu nyingine.

“Awali nilisema kuwa kuna timu ambazo zilionyesha nia ya kutaka kumsajili moja ya nje na nyingine za hapa ndani na tunasaini mkataba wa awali huku tukisubiri majibu ya Simba ingawa kwa sasa wakitupa barua ndiyo itakuwa vizuri zaidi,” alisema Ndambi ingawa habari zinamhusisha mchezaji huyo na Kaizer Chief ya Afrika Kusini.

SOMA NA HII  AZAM FC YAZIWEKA KANDO SIMBA NA YANGA KWA MTINDO HUU