Home Uncategorized MWAMBUSI ARUDI MBEYA CITY, ASAINI MWAKA

MWAMBUSI ARUDI MBEYA CITY, ASAINI MWAKA


KOCHA Juma Mwambusi amerejea nyumbani pale Mbeya City na kusaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuinoa timu hiyo msimu ujao.

Mwambusi ndiye aliyeipandisha daraja Mbeya City na msimu wa 2013/14 wakashiriki ligi kuu na kutoa upinzani wa hali ya juu na kumaliza ligi wakiwa nafasi ya tatu kisha akatimka kikosini humo msimu wa 2015/16 na kujiunga Yanga.

Katika msimu ulioisha wa 2018/19 Mwambusi alikuwa kocha msaidizi wa Azam FC chini ya Mholanzi Hans van Der Pluijm ambao walitimuliwa kufuatia matokeo mabaya ambayo timu hiyo ilikuwa ikiyapata.

Mwambusi alisema: “Nimesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia Mbeya City kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu baada ya kufikia makubaliano na uongozi, hivyo nimeamua kurudi kuifundisha timu yangu ya awali.

“Nitahakikisha timu inafanya vyema msimu ujao kama ilivyokuwa huko nyuma.”

SOMA NA HII  SINGIDA YA KIMATAIFA NJE YA DIMBA