Home Uncategorized STRAIKA SIMBA ASAINI AFRIKA KUSINI

STRAIKA SIMBA ASAINI AFRIKA KUSINI


MSHAMBULIAJI wa Simba, Adam Salamba ametua rasmi katika kikosi cha TS Sporting ya Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Salamba alisajiliwa na Simba msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Lipuli FC ya Iringa kwa dau la Sh mil 30 na gari.

Awali iliripotiwa kuwa, Salamba angejiunga na Klabu ya Polokwane City ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini kuchukua nafasi ya John Bocco ambaye alikuwa akitakiwa na klabu hiyo.

Habari za ndani kutoka Simba zinadai kuwa, mshambuliaji huyo klabu imemtoa kwa mkopo kwenda TS Sporting ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Afrika Kusini kwa mwaka mmoja. Kiliongeza kuwa, Salamba tayari ameanza mazoezi na klabu hiyo na msimu ujao atakuwa hapo.

“Salamba ni rasmi msimu ujao atakuwa Sauz akicheza katika Klabu ya TS Sporting kwa mkopo kwenye klabu hiyo na sio Polokwane City kama ilivyokuwa awali,” kilisema chanzo. Kwa upande wake Salamba alithibitisha:

“Ni kweli nipo Sauz kwa sasa lakini mambo ya timu yangu mpya kwa sasa siwezi sema, nikikamilisha nitakueleza nini kinaendelea.”

SOMA NA HII  BEKI SIMBA SASA AGEUKIA MAPISHI