Home Uncategorized YANGA YAMFICHA HOTELINI STRAIKA SIMBA

YANGA YAMFICHA HOTELINI STRAIKA SIMBA


UNAMKUMBUKa yule straika ambaye Simba ilitangaza kumsajili kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19?

Straika huyo si mwingine bali ni Vitalis Mayanga aliyekuwa Ndanda FC ambaye katika msimu wa 2018/19, aliwafanya vibaya Yanga katika mechi zote mbili walizokutana zilizomalizika kwa sare ya 1-1.

Mayanga katika mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, aliwapiga chenga mabeki wote wa Yanga na kipa wao, Beno Kakolanya kabla ya Nassor Hashim kufunga kirahisi, huku bao la Yanga likifungwa na Jaffary Mohammed.

Mechi ya pili, Mayanga aliifungia Ndanda bao moja katika sare ya 1-1.  Bao la Yanga lilifungwa na Papy Tshishimbi. Sasa baada ya kufanya balaa hilo, Yanga katika kukisuka zaidi kikosi chake kwa msimu ujao, kimemfuata straika huyo na muda wowote atapewa mkataba na wamemficha hotelini maeneo ya Sinza.

Mtu wa karibu na Mayanga ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Mayanga na Yanga mambo freshi kwani hivi tunavyoongea leo ni siku ya tatu amefichwa katika moja ya hoteli jijini Dar, muda wowote watamalizana.”

Championi lilimtafuta Mayanga kuthibitisha hilo ambapo alisema: “Mkataba wangu na Ndanda umemamalizika, hivyo nipo huru kujiunga na timu yoyote, bado sijasaini Yanga lakini wakinipa maslahi mazuri sikatai. “Lakini hiyo ishu ya mimi kuishi hotelini wala lisikutishe, kwani mimi nani mpaka nisikae hotelini, wewe subiri mambo yakikaa sawa utafahamu tu.”

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, aliliambia Championi Jumatano kuwa: “Kwa sasa tupo bize na usajili wa wachezaji wa kimataifa, tushawasajili wanne, hivyo suala la wachezaji wa ndani ni hapo baadaye.”

CHANZO: CHAMPIONI

SOMA NA HII  WALIOPIGWA MBILI NA SIMBA WASAJILI WAPYA SITA