Home Uncategorized YANGA YASAJILI BEKI AFCON

YANGA YASAJILI BEKI AFCON


HATIMAYE ahadi ya Waziri wa zamani na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba imetimia baada ya kuzama mfukoni kwake na kufanikisha usajili wa beki kisiki wa Lipuli na timu ya taifa, Taifa Stars, Ally Mtoni ‘Ally Sonso’.

Mwigulu amefanikisha usajili huo ikiwa ni sehemu ya ahadi yake kwa Wanayanga ambapo aliahidi kuwasaidia kusajili mchezaji mmoja wa ndani atakayependekezwa na benchi la ufundi hivyo pesa yake imetumika kumsajili mchezaji huyo.

Chanzo cha habari hii kimelinyetishia Championi Jumatano kuwa, tayari Mwigulu ametimiza ahadi yake kwa kufanikisha usajili wa Ally Sonso, hivyo hadaiwi lolote kwani pamoja na kwamba mchezaji huyo hajatangazwa hadi sasa ila ukweli ni kwamba uwepo wake Yanga msimu ujao umewezeshwa na yeye.

“Tunashukuru baadhi ya ahadi za wadau wetu zimezidi kufanywa kama ilivyopangwa, ambapo utaona kati ya wengi walioahidi kuisaidia Yanga katika suala la usajili wamefanya.

“Ahadi ilitolewa na Mbunge huyo ni kwamba atasajili mchezaji mmoja wa ndani na tayari ameshakamilisha hilo kwa kumsajili Sonso na kilichobaki kwa sasa ni kutambulishwa tu,” kilisema chanzo hicho.

Taarifa zinasema kuwa Mwigulu alimtuma mmoja kati ya wabunge kwenda kwenye kambi ya Stars nchini Misri hivi karibuni na kumalizia mazungumzo machache yaliyokuwa yamebaki na hivyo dili hilo limekamilika.

SOMA NA HII  BOSI WA AZAM FC KUKUTANA NA MWANAFUNZI WAKE WA ZAMANI LEO